John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 296
- 103
| Miradi | 2020 | 2025 | Ongezeko |
|---|---|---|---|
| Idadi ya vikundi vyote | 187 | 324 | 137 |
| Vikundi vya wanawake | 92 | 99 | 7 |
| Vikundi vya vijana | 53 | 139 | 86 |
| Vikundi vya wenye ulemavu | 42 | 86 | 44 |
| Thamani ya mikopo (TSh Bil.) | 1.63 | 5.88 | 4.25 |
| Wanufaika TASAF | - | 50,934 | - |
| Wanufaika leseni za madini | - | 1,836 | - |
| Jumla ya wanufaika wote | - | 52,770 | - |
| Jumla ya fedha zote (TSh Bil.) | - | 5.88 | - |
KAZI IMEPIGWA KWELI KWELIAsante Sana Mheshimiwa
Tasaf ni fedha za mkopo toka Bank ya Dunia.==
Katika sekta ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Sita imetoa miongozo ya kuyawezesha makundi mbalimbali ya jamii kuimarisha uwezo wao wa kushiriki shughuli za maendeleo na kuleta usawa wa kiuchumi. Katika kipindi hiki, kumekuwa na ongezeko la vikundi vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri za Mkoa wa Mara kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kutoka vikundi 187 mwezi Novemba 2020 hadi vikundi 324 Aprili 2025. Fedha zinazotolewa kama mikopo kwa vikundi hivyo zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.63 Novemba 2020 hadi shilingi bilioni 5.88 mwaka 2025.
Idadi ya vikundi vya wanawake imeongezeka kutoka vikundi 92 Novemba 2020 hadi vikundi 99 Aprili 2025, vikundi vya vijana kutoka 53 hadi 139, na vikundi vya watu wenye ulemavu kutoka 42 hadi 86. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na vikundi hivi ni pamoja na kuongezeka kwa ajira, kuimarika kwa uchumi wa vikundi na mtu mmoja mmoja, pamoja na kupungua kwa utegemezi wa makundi haya katika jamii. Kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mkoa wa Mara una jumla ya wanufaika 50,934 hadi Juni 2025, ambapo wananchi hao wameweza kuboresha maisha yao kwa kujifunza na kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Aidha, Mkoa kwa kushirikiana na Tume ya Madini na Mgodi wa Barrick North Mara umewawezesha upatikanaji wa leseni 104 kwa vikundi 48 vyenye jumla ya vijana 1,836 kutoka vijiji 13 katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime. Uwezeshaji wa makundi hayo ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT) yenye lengo la kutoa fursa kwa vijana kushiriki katika mnyororo wa thamani wa madini. Vijana hao wanapatiwa elimu kuhusu uchimbaji wa madini chini ya uangalizi wa Mgodi wa Barrick North Mara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Ofisi ya Madini Mkoa.
Hata hivyo fedha zote zilizotamkwa katika utekelezaji wa miradi ya uwezeshaji ni shilingi bilioni 5.88, huku jumla ya wanufaika wote wakiwa watu 52,770.
Miradi 2020 2025 Ongezeko Idadi ya vikundi vyote 187 324 137 Vikundi vya wanawake 92 99 7 Vikundi vya vijana 53 139 86 Vikundi vya wenye ulemavu 42 86 44 Thamani ya mikopo (TSh Bil.) 1.63 5.88 4.25 Wanufaika TASAF - 50,934 - Wanufaika leseni za madini - 1,836 - Jumla ya wanufaika wote - 52,770 - Jumla ya fedha zote (TSh Bil.) - 5.88 -
sawa ila chini ya Rais samiaTasaf ni fedha za mkopo toka Bank ya Dunia.
Aliyekopa hizi ni Jiwesawa ila chini ya Rais samia
KWANINI UFE KWA PRESSUREHaya matapeli ukiyasikiliza unaweza kufa na pressure bure
Yanaiba mpaka yanakeraKWANINI UFE KWA PRESSURE
akina nani?Yanaiba mpaka yanakera
Tangu enzi za JK, TASAF ilishakuwepo, ikaja enzi za JPM TASAF ilikuwepo hadi kipindi hiki ipo. Halafu TASAF sio mradi wa hizo billion 2 hadi 6 unzotaja, huo mradi unafika hadi trillion kadhaa na hakuna alichoongeza Wala kupunguza Samia. Na kwenye hii thread yako umeitaja TASAF mara moja tu wakati kichwa Cha habari kinahusu TASAF. Kama hamna taarifa sahihi na za kutosha msiwe mnaanzisha nyuzi na kusubiri kupata elimu kwenye comments. Akipita hapa mtu anayefanya kazi TASAF atakuona kama CHAWA pro-max kiwango cha LUCAS Muwashambwa.akina nani?
kwa mkoa mmoja> au unazungumzia nchi nzima?Tangu enzi za JK, TASAF ilishakuwepo, ikaja enzi za JPM TASAF ilikuwepo hadi kipindi hiki ipo. Halafu TASAF sio mradi wa hizo billion 2 hadi 6 unzotaja, huo mradi unafika hadi trillion kadhaa na hakuna alichoongeza Wala kupunguza Samia. Na kwenye hii thread yako umeitaja TASAF mara moja tu wakati kichwa Cha habari kinahusu TASAF. Kama hamna taarifa sahihi na za kutosha msiwe mnaanzisha nyuzi na kusubiri kupata elimu kwenye comments. Akipita hapa mtu anayefanya kazi TASAF atakuona kama CHAWA pro-max kiwango cha LUCAS Muwashambwa.
Majangili ya mali za ummaakina nani?
kwanini usiwakamate?Majangili ya mali za umma
Mahakama na polisi ni mashina ya UVCCM utaenda kuwafunga na nini?kwanini usiwakamate?
njoo CCM acha kujitesa ndg yanguMahakama na polisi ni mashina ya UVCCM utaenda kuwafunga na nini?
Siwezi kuungana na majangili ya mali za ummanjoo CCM acha kujitesa ndg yangu
HAIWEZI KUTOKEASiwezi kuungana na majangili ya mali za umma
Endeleeni kuiba mali za ummaHAIWEZI KUTOKEA
wewe unaiba za nani huko CHADEMA?Endeleeni kuiba mali za umma