Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Wakazi wa kata ya Mvuleni, manispaa ya Lindi wameeleza watakavyonufaika na uwepo wa kituo cha afya cha kisasa kilichojengwa kutokana fedha za tozo za miamala ya simu kikiwa na thamani ya Sh250 milioni.
Kabla kituo hicho hakijajengwa wananchi walilazimika kwenda kufuata huduma za afya katika kijiji cha Kitomanga wakitembea umbali wa zaidi ya saa moja au zaidi na wakati mwingine walilazimika kwenda mjini umbali wa kilomita 65.
Mkazi wa Mvuleni – Mashariki, Hadija Nampamba alimshuruku Rais Samia kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo, akisema hapo awali walikuwa wakihitaji huduma iliwalazimu kupitia changamoto mbalimbali ili kufanikisha matibabu.
“Zamani mtu akipata ujauzito wanafunga matenga kwenye baiskeli au pikipiki wakupeleke katika hospitali ya Sokoine iliyopo Lindi mjini. Wakati mwingine kina mama wanajikuta wanajifungulia njiani kutokana na umbali wa hospitali au kupoteza maisha na mtoto.
“Hii ilikuwa adha kubwa kwa kina mama lakini tunaishukuru Serikali yetu kwa kutujali na kutusogezea huduma hii. Sasa hivi zile adha za kuelekea zahanati ya Kitomanga au Lindi Mjini zitapungua, hiki kituo kipo karibu na unatembea muda mchache sana,” alisema Hadija.
Hadija alitolea mfano miaka ya nyuma mdogo wake mjamzito aliposhikwa na uchungu, walimuweka kwenye tenga na kupakiwa kwenye pikipiki kumsafirisha hadi Lindi mjini ambako hata hivyo, ndugu yake huyo pamoja na mtoto walifariki dunia.
Mkazi wa Kijiji cha Maloo kichopo ndani ya kata Mvuleni, Kazibure Abdallah aliishuruku Serikali kwa ujenzi wa kituo cha afya, akisema kimeanza kutoa huduma kinaupunguza umbali wa kutembea hadi kijiji cha Kitomanga ambapo gharama yake Sh 10,000.