Fedha zetu za Michango ya ujenzi wa uwanja wa Simba ndio zimeliwa?

utopolo og

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
575
Reaction score
1,575
Aliyekuwa mtendaji mkuu wetu aliyepita ndugu Barbara alianzisha harambee ya kuchangisha Fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja chetu ambapo mwekezaji wetu alitoa bilioni 2 kama mchango wake binafsi.
Wanasimba wengi tulichanga kwa fujo Fedha ili tuweze kumiliki kiwanja chetu Cha kuchezea mechi zetu mbalimbali.

Sasa ni zaidi ya miaka mitatu hatusikii chochote kutoka kwenye uongozi kuhusu hatma ya Michango yetu, Je ndio kusema Fedha zetu zimeliwa??

Wanasimba wenzangu mbona mmelala? Watu wanatafunaa Fedha zetu nanyinyi mpo kimya tu?

Naomba waziri wa Michezo, Sanaa na utamaduni uingilie kati hili suala maana Fedha zetu zinatuuma

Cc: Aden Rage
 
Ila twende mbele turudi nyuma, hizi Simba na Yanga zina mashabiki wanafki sana kama wale wa Hip Hop ngumu, kazi kusifia punchlines tu, mara unasimania nguzo blah blah. Andaa Shoo huwaoni toa Albam hawanunui.

Wanachama wamepewa asilimia nyingi kuliko Mo lakini ni wangapi wanalipia ada ya uwanachama. Wengine hata jezi tu wananua zile feki halafu bila aibu anaingia nazo uwanjani. Wanalazimamisha timu isajili wachezaji wa daraja la juu, ukiwawekea kiingilio cha hata efu 10 tu mzunguko wanalalamika maisha ya Mtanzania. Kama mnaona maisha ya Mtanzania magumu kwanini mlazimishe mtu mmoja afanye kila kitu na nyie wanachama.

Nina uhakika zile hela zilizochangwa hata nusu ya robo ya lengo hazikufika.
 
Hawa si ndio aina ya walioambiwa wamevimbiwa mihogo na Rais wa mwiko nyuma.Hamna agenda mpya sasa lazima ianzishwe.Wenzenu wana hata pa kufanyia mazoezi nyie tia mchuzi pangu pakavu hata cha kufugia samaki kiliwashinda.Walizoa matope limebaki korongo.
 
Pamoja na kukashifu hao wanachama, kwanini wanaojiita wasomi au wenye uwezo wasiige mfano wa bakhresa na kuanzisha timu zao.
 
Hamjui kuwa watu maskini ndo fursa?Yaani ukiwaambia watu million 60 watoe elfu moja moja tu,hapo tayari una M60.Poleni mnaowachangia matajiri.Mnajua mnachangia uwanja kumbe mnamchangia Mmwamedi.

Uwezo wako wa kuandika hayo ungeenda kwanza kusomea hesabu ingekusaidia sana yani watu million 60 wakitoa 1,000 inakuwa million 60 Kajifunze hesabu kwanza
 
Bila unafiki, sema ktk hizo fedha wewe ulichangia TSH ngapi. Na he uwanja huo unagharim TSH ngapi. Ukijib hayo hata MO lazima awe mpole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…