gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 790
- 1,373
Tunapo karibia uchaguzi mkuu pesa itatafutwa kwa njia yoyote ile ikiwemo ya halali na ya haramu. Hatuwezi kupuuzia jambo dogo kama hili la kubadilisha fedha ambazo kimsingi zilisha pita muda wake wa matumizi, ni fedha zilizo kwisha ku-expire.
Nadhani ni fedha ambazo hazipaswi kurudishwa tena kwenye mzunguko. Ninavyo fahamu mimi kabla ya ku introduce note mpya tangazo lilipita na watu wakazibadilisha note hizo, inakuwaje tena sasa ionekane kuwa note hizo bado zina thamani ile ile ya tangu miaka ya 95 ama 2003?
Kutokana na kufikiria kwa kina nimehisi hapa kuna harufu ya utakatishaji fedha, na kutokana na maoni ya wadau mbalimbali nimegundua vitu kadhaa.
(i) Ni fedha ambazo watu walizificha kwenye masandarusi na mahandaki na sasa wanatumia mwanya wa kuzirudisha ili wapewe fedha halali na wazirudishe kwenye mzunguko.
(ii) Ni fedha zilizoibwa kwenye mambenki ambazo zilisha pita na muda wake na wahusika wakitumia njia ya kuzihalalisha ili zirudi kwenye mzunguko.
(iii) Ni fedha halali na inafaa zirudi benki ili zifutwe kabisa na kupatikana fedha mpya. (Hii ni kwa maono ya BOT wenyewe)
Kwa maoni yangu mimi hapa kuna harufu ya ufisadi mwingine unao enda kutokea. Tusijifunze kupuuzia kila jambo, jambo hili laweza kuonekana kuwa dogo lakini likawa na impact kubwa hasa kwenye uchumi wa nchi yetu kwani kitaalamu hatuelewi ni idadi kiasi gani ya fedha hizo ambazo hazikubadilishwa kwa sababu kadhaa ikiwemo hofu ya kukamatwa ama kutaifishwa.
Iwapo zikiwa ni chache haziwezi kuwa na athari kubwa lakini iwapo zikiwa ni ma billions ya shilingi inaweza kuleta changamoto hasa kwenye uchumi wa nchi yetu. Isije ikawa nia hii njema ya BOT ikaingiliwa na watu wasio kuwa na nia njema na hasa wenye nia ya kutakatisha fedha.
Tujadili bila kutumia personal attacks, twende hoja kwa hoja lengo ni kueleweshana.