Fedha zinapotumika nje ya bajeti, Bunge letu "tukufu" na Kambi ya Upinzani vinakuwa wapi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Kwa kifupi sana ningependa kujua nini maana ya "fedha za serikali zimetumika nje ya bajeti"?

Ninavyojua moja ya kazi kuu ya Bunge ni kusimamia serikali, sasa inakuwaje bunge lipitishe bajeti iliyowasilishwa na serikali halafu bajeti hiyo isiheshimiwe na watendaji wa serikali?

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) hana nyenzo za kubaini ufisadi wa serikali?

Mbona Dr Slaa, Zitto Kabwe na Kafulila walikuwa mwiba wa serikali?

Tutaibiwa kodi zetu hadi lini?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Wanakuwa kwenye pambio za sifa, hivyo yaweza kuwa sii kosa lao ila kwakuwa ni katikati ya pambio za sifa mengine yanawapita.
 
Ulitaka wapinzani wakamshike mashati rais? Wa kulaumu ni mibunge ya ccm
Upinzani unaingiaje hapo wakati bado mna kampeni ya kuangamiza wenye mawazo mbadala,na mlishajaribu Sana mkashindwa,na bado mnajitutumua kuuua kwa mujibu wa matendo na hata matamshi yenu.
 
Upinzani unaingiaje hapo wakati bado mna kampeni ya kuangamiza wenye mawazo mbadala,na mlishajaribu Sana mkashindwa,na bado mnajitutumua kuuua kwa mujibu wa matendo na hata matamshi yenu.
Hakuna mpinzani bungeni wote ni CCM
 
Wale kina covid 19 hawajaanzisha kambi Rasimi ya upinzani?
 
Hiyo ni miezi 3 tu nje ya bajeti,malipo Mara mbili zidisha Mara miaka 5.
Ndege zilikuwa zinaidhinishwa na bunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…