Kwa kifupi sana ningependa kujua nini maana ya "fedha za serikali zimetumika nje ya bajeti"?
Ninavyojua moja ya kazi kuu ya Bunge ni kusimamia serikali, sasa inakuwaje bunge lipitishe bajeti iliyowasilishwa na serikali halafu bajeti hiyo isiheshimiwe na watendaji wa serikali?
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) hana nyenzo za kubaini ufisadi wa serikali?
Mbona Dr Slaa, Zitto Kabwe na Kafulila walikuwa mwiba wa serikali?
Tutaibiwa kodi zetu hadi lini?
Nawasalimu kwa jina la JMT!