Feedback FEEDBACK..!

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2007
Posts
9,346
Reaction score
3,028
Habari zenu wana Jf!

Niliweka tangazo humu la kutafuta girlfriend, siku hiyo hiyo nilimpata.

Tukaonana, bada ya siku tatu akaanza kuomba pesa, siku ya kwanza nilimpa kama elfu sabini na tano, alisema mama ake anaumwa mala ya pili akaomba kilo, leo asubuhi tena kaomba laki tatu. Ukweli kimuonekano ni binti mrembo na ni mzuri kweli yani na anafaa kua mke.

Haya ndio yaliyo nikuta, na watu kama hawa ndio wana haribia wengine hadi tunakua tunaogopana.
 
Sasa na wewe ulikubali vipi kumpa pesa bila kumuona mama yake hujui kama kuna matapeli wa mapenzi? Kakuona kuwa umekuwa teja kwa uzuri wake ndo maana kakufanyia hivyo. We mtu hata hujazoeana nae kihivyo yani zimepita siku tatu tu anakuomba pesa hugutuki? Kaka kama unaangalia uzuri basi msubirie tu ila kama watafuta mke mwema huyo hakufai kwanza hana hata mpango nawe.
 
huyo anakutaka kwa mambo yake binafsi na hana upendo wa dhati. achana nae
 
pole sana yametukuta wengi hupo peke yako ila sie wagumu kwani hadi watoto tuliambiwa wanaumwa kama tulizaa naye mara viatu vinabana yaani ni ushamba tu, jitu zima akili matope kaona namtosa hela kapotea hawa mabinti ukiwachekea watakumaliza kuwa makini sana
 
Siku hizi si mabinti tu hata vijana nao wanapenda pochi tu.
 
Uwe unafikiria kwanza, kama huna cha ku post katika uzi unaupita kama ulivyo, wewe u comment au usi comment tunajua upo bana.. Mnakera sana mnao force kuandika neno kwenye thread hata kama huna la maana
No comment..
 
Mie, nilimuamini the way hata alivyo jielezea nikajikuta nina mpa. Kwa kuweka thread hii ndio mwisho wake maana najua ameiona hii thread
 
Kwa mfumo huu wa maisha, hadi tutakua tunaogopana ndugu, yani watu wameweka pesa mbele kuliko utu wao..
 
ah ah..! utapeli @ work

Ila wewe inaelekea una pesa nyingi na hazina kazi..! Yaani msichana humjui vizuri kurupu kurupu unampa elfu sabini na tano, mara kilo.! Mh.... Ngoja nami niku PM namba yangu ukiipata tuu unitumie LAKI MBILI..!
 
Kha! sasa kama unayo na mtu kakuambia anashida haina budi kumsaidia, ila kama ile pesa anaitumia kwa mambo mengine tofauti na aliyoombea ndio inakera

Muwe mnasoma alama za nyakati .! Siku zote asipate shida aje kupata shida siku mbili baada ya kukufahamu..! Aaaah...
 
Mie, nilimuamini the way hata alivyo jielezea nikajikuta nina mpa. Kwa kuweka thread hii ndio mwisho wake maana najua ameiona hii thread

Kaka yangu kwa jinsi mapenzi siku hizi yalivyo ni kama sinema usithubutu kutanguliza pesa mwanzoni. Inavyoonekana alishakusoma akajua unazo. Mwanamke gani siku ya tatu tu ushaanza kuomba hata haya hana kha!
 
Ila kweli dah! Hapa nimejifunza sitorudia tena kosa la na mna hii..
Muwe mnasoma alama za nyakati .! Siku zote asipate shida aje kupata shida siku mbili baada ya kukufahamu..! Aaaah...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…