Fei Toto anapaswa kuangalia upya mstakabali wa maisha yake ya soka

Fei Toto anapaswa kuangalia upya mstakabali wa maisha yake ya soka

pakacha77

Member
Joined
Aug 12, 2022
Posts
91
Reaction score
98
Juzi kabla ya marejeo(Review) ya kesi ya Fei Toto dhidi ya Young Africans kuna baadhi ya wachambuzi nzala walimhoji kwa makusudi Mama yake Fei Toto ili kuishinikiza kamati ya TFF inayohusika na kesi hiyo ije na matokeo tofauti na yale ya awali eti tu kwa kuwa Mama yake analalamika kuwa mwanae anaonewa na kusahau kwenye mambo ya kimkataba.

Public sympathy haiwezi kusaidia zaidi ni kushindana kwa hoja . Kama Fei Toto na washauri wake wameamua suala liende kisheria wacha iwe hivyo asitokee mtu na kusema eti Yanga wavae uhusika WA mzazi dhidi ya mtoto aliyekosea kwa sababu anaonyesha kiburi cha wazi kabisa mbaya zaidi hata Mama yake amejiingiza rasmi kumtetea mtoto wake huku akiukataa ukweli.

Hapa ni jino kwa jino mpaka mwisho wa mkataba wake utakapotamatika 2024 ndio aende timu nyingine akiwa mchezaji huru.

Yanga ni taasisi huwezi kushindana nayo yeye hachezi lakini timu inapanga mipango yake na inashinda.
 
Yuko sahihi. Mwisho km huu ataki
IMG_7853.jpg
 
Acha dogo apiganie maslahi yake.... atafute hela kabla uzee haujamfika
 
Back
Top Bottom