Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Kwa mara nyingine naona Bwana Fei Toto kawasilisha barua TFF ya kutaka kuvunja mkataba na Yanga. Mpaka sasa nafikiri yeye na watu wake washashtuka na kuona kuna mahala waliteleza ndio maana wanakwepa kupeleka mashtaka CAS.
Kwa akili ya kawaida baada ya review yake kugonga mwamba, alitakiwa anyooke CAS moja kwa moja kama alikuwa anaona hajatendewa haki, na anaona alichokifanya alikuwa sahihi kwanini tena awasilishe barua nyingine wakati anadai ameshavunja mkataba na waajiri wake?
Hiki ni kichekesho kingine anapeleka barua TFF, kwani TFF ndio waajili wake? TFF inawezaje kuvunja mkataba wake wakati washamwambia ni mchezaji halali wa Yanga? Anajaribu kuwakwepa Yanga lakini hatoweza, ni mpaka atarudi kwao tu.
Hata akiruka akaenda wapi, TFF watamwambia aende akaongee na waajiri wake na si vinginevyo, kiburi chake hakiwezi kumsaidia hata alete Wanasheria kutoka Sayari ya Mars hawezi toboa kwa staili anayotaka yeye.
Kuongea na Yanga hakuepukiki, aende wamtajie dau lao la kuvunja mkataba endapo watakubaliana na sababu anazozitoa na si vinginevyo, na ziwe sababu zilizoshiba zinazoendana na muongozo wa mikataba ya FIFA otherwise haitokuwa rahisi pia.
Dawa ya kiburi ni jeuri, asisahau hilo.