Fei Toto kwenda Azam sports club na hadithi za kobe aliyejificha kwenye nyumba yake

BETONY

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
188
Reaction score
170
Ni ukweli usiopingika kuwa Fei Toto amekuwa moja ya wachezaji muhimu sana Yanga. Na ni ukweli kuwa kijana amekuwa akiipambania Yanga kwa jasho na damu kwa kipindi chote alichokuwa anaichezea timu hii ya Jangwani.
Hakika litakuwa pigo kwa Yanga, lakini kuna msemo unasema "watu uja na kuondoka" na huu ni wakati wa Yanga kuachana na Fei Toto.
Taratibu za kimkataba zinatakiwa kufuatwa kwa pande zote mbili kurudi kwenye misingi ya kimkataba na kupata majadiriano ya pamoja.
Kwenda Azam sports club kwa Fei Toto nadhani ni kurudi nyuma kwake, japo kimaslahi inawezekana ikawa na faida kwa upande wake.
Kipindi hiki Azam imetumia njia moja ama nyingine kuivuruga Yanga nje ya uwanja. Kwa hesabu za Azam ni ukweli uliowazi kuwa wasingiweza kuikuta Yanga. Hiki walichokifanya nyuma ya pazia kwa kumlipa kinyemera Fei hili aweze kuondoka Yanga kinafaa kupigwa vita na wote wanopenda maendeleo ya mpira nchini. Kama walikuwa na nia ya dhati ya kumtaka Fei Toto wangepitia mkataba wake na Yanga na kwenda kuongea na wamiliki halili wa mchezaji na sio kutumia mbinu hii chafu ya kumlaghai mchezaji.
Kwa hakika Azam watakiwa kulaaniwa na kila mwanamichezo kwani wameukosea sana hemshima mpira wa miguu na wameikosea sana Yanga.
Dunia kote mkataba unavunjwa na pande mbili na siyo hiki halichokifanya Fei Toto.
Yanga kiutaratibu wanatakiwa kwenda kisheria, na hii ya kulinganisha mishahara baina ya wachezaji ni ujua wetu sisi. Mshahara unajadiliwa na pande mbili na kama ukikubari ma kusaini haitakiwi kujiringanisha na wengine. Ni mara nyingi sana mnaweza kuwa mnafanya kazi moja na pengine wewe ukawa unafanya kazi kubwa zaidi, lakini mwenzako hakakuzidi mshahara. Angalia mfano wa wafanyakazi wa kampuni, lengo la kampuni yoyote ni kupata kingi, wakati matumizi yakiwa kidogo. Yanga haina kosa kumlipa Fei Toto kiwango hicho, kwani yeye mwenyewe alikiridhia na kusaini.
Wachezaji wetu wanatakiwa kujifunza katika ku bargain vipengele vya mikataba na siyo kutia huruma kuwa mimi nalipwa kidogo kulingana na kazi nayofanya.
Azam waache hujuma za nje ya uwanja, wapambane ndani ya uwanja.
Kila la kheri Fei Toto, lakini tekeleza matakwa ya mkataba wako na Yanga, kama kuna timu inakuhitaji inatakiwa kukaa chini na Yanga na kuzungumza na si huu uhuni wa miaka ya 90.
 
tatizo la fei toto ni kukosa elimu
 
tatizo la fei toto ni kukosa elimu
Na hii ni shida kwa wachezaji wengi wa kitanzania, mwisho wanakuwa na wivu na maneno ya kiswahili, ohhoo, napiga kazi mshahara kidogo, wakati wengine mshahara mkubwa. Je wakati unasaini ulikuwa wapi ku bargain hili upate mkubwa?
 
Na hii ni shida kwa wachezaji wengi wa kitanzania, mwisho wanakuwa na wivu na maneno ya kiswahili, ohhoo, napiga kazi mshahara kidogo, wakati wengine mshahara mkubwa. Je wakati unasaini ulikuwa wapi ku bargain hili upate mkubwa?
Wakati anasign alikuwa mchezaji wa kawaida sasa kiwango kimekua
 
Mwacheni dogo anende pesa ndio rafiki wa kweli, life goes on. Daima mbele
SASA HUU UKIWA NDO UTARATIBU SI KILA WACHEZAJI WATAKUWA WANAONDOKA TU AKIPATA SEHEMU YA MSHAHARA MKUBWA.

KWANI MASLAHI YA VILABU HAYATAKIWI KULINDWA???

Unachokaanisha hata kama klabu nazo zinaina huna kiwango zinaamua tu kukuacha na kuvunja mkataba bila maridhiano??

Au kwenye mikataba wenye haki ni wachezaji tu??

Ukiweza tujadili tusikebehiane kinazi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…