Fei Toto kwenda Azam sports club na hadithi za kobe aliyejificha kwenye nyumba yake

Pesa atapata lakini...
... ndiyo mwisho wake kimpira.

Yaani ukitoka Yanga au Simba huwezi kwenda kucheza timu zaidi ya hizo ukanawili na kuuzwa nje ya nchi.

Fei atapata pesa ila kimpira ndiyo kwaheri!.
 
Kwani hana wakala au mwanasheria wa kumwakilisha? Kwamba kaenda front mwenyewe kuchukua fedha Azam? Athletes wote duniani kwa sasa wanatazama maslahi kwani umri unasonga na baada ya muda hawatakua na peak walizonazo kwa sasa hivyo ni lazima wawe opportunist. Mfano mzuri Sadio Mane kutoka Liverpool kwend Beyern Munich etc.

Sina ushabiki wa club yoyote Tz usibebe hili kishabiki.
 
Kwahiyo mtoa post unalia Fei Tofo kuondoka?
 
Na huu ndo ukweli.Hata ningekuwa mimi kama nimepata ofa nzuri na maslahi mazuri naondoka jata kama timu ilinitibu UKIMWI
Pesa pesa pesa.Tafuteni pesa mengine mtazidishiwa,😂😂😂😂😂😂
 
Hebu tukumbushane kidogo maana binadam tumeumbwa kusahau, ivi wakati ule MSHERY anasajiliwa pale Jangwani watu (Timu) walikaa meza ipi hiyo?....
Issue ile na ya MSHERY na hii ni tofauti kabisaaaa! Msikilize wakala wa Mshery alishalitoa maelezo, yanga, Mtibwa na Mshery walikaa meza moja kujadiliana mtibwa wakatoa mapendekezo yao yalipotimizwa ndo wakatoa ruhusa dogo kuondoka ingekuwa kinyume basi Tff wasingetoa kibari. Sema kwenye kulipana kati ya Yanga na Mtibwa ndo ikatokea kuchelewesheana wakati dogo alishaanza kuitumikia yanga

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kumbe ilikua hivyo unaanza kumtumia mchezaji kabla ya ktmalizana afu ikaonekana ni sawa tu, kisa wale ni Mtibwa FC.
Haya tuje kwenye mfano unaendana sasa japo kwa % kadhaa... Ivi ule uhamaisho wa Neymar Jr kutoka Barcelona kwenda PSG kwani timu zilikaa meza ipi kufanya maridhiano ya kumnunua Neymar.
Yani kama nakiona kitengo cha sheria na suti zao wakifanya makosa tena, muda huu wajipange vizuri aisee maana BARCA na ukubwa wao wamewahi kufeli kwenye hili...
 
Kasome kanuni za FIFA kwanza kuhusu kuvunja mkataba. Ni kweli mpira ni pesa lakini afuate taratibu zote alizokubali wakati anasaini mkataba wake
 
Mkuu kwani unadhan Fei hana wanasheria?
Ama unadhani Azam hawakufiri Kama ulivyofikiri?
Uyanga wenu na usimba ndio inaoowaangusha, mchezaji mkimtaka nyie mnatumia umafya mkifanyiwa nyie mnaona mmeonewa. Ngoja dogo ale ice cream kidogo acha wivu.
 
Kasome kanuni za FIFA kwanza kuhusu kuvunja mkataba. Ni kweli mpira ni pesa lakini afuate taratibu zote alizokubali wakati anasaini mkataba wake
Kwani hizo kanuni unazotaka nikasome zimewekwa baada ya uhamisho wa Neymar.... Kama timu kubwa na iliyokua na ushawishi mkubwa FIFA walifeli kumbakiza Neymar sijui kwa Yanga, kama hizo kanuni zimekuja baada ya uhamisho wa Neymar... Halafu kumbe Yanga walishaanza mazungumzo na mchezaji kuhusu maboresho ya mkataba wa mchezaji basi bila shaka hawajaafikiana ndo maana mchezaji kaamua kuununua mkataba na hatimaye kuuvunja sasa apo sijui meza ipi Yanga wanataka wakae ikiwa wamekaa na mchezaji kwaajili ya marekebisho na imeshikana au mimi ndo sijaelewa taarifa yao wailiitoa Yanga.
 
Kasome kanuni za FIFA kwanza kuhusu kuvunja mkataba. Ni kweli mpira ni pesa lakini afuate taratibu zote alizokubali wakati anasaini mkataba wake
Mkuu umekazana na kuvunja tu mkataba.

Kwani sheria inaelekeza vipj kuhusu kuununua mkataba na kuuvunja naona tu umekazana hajafuata sheria, sheria ipi?
Halafu swali lingine inamaana fei na azam hawajasoma terms za contract mpaka wakurupuke hivyo?.
 
Sawa ndio mumpe feisal million nne kama anacheza geita gold kazi yenu dhulma yaani hapo mshampeleka kwa babu ili afeli kama ajibu na gadiel miko
 
Hakuna ambaye hanamzuia kwenda Azam, kikubwa ni kuheshimu vipengele vya kimkataba basi
Wewe mkataba wake umeuona wapi au wewe ni msemaji wa Yanga,tuliza boli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…