Feisal amevuta milioni 90 kutoka kwenye klabu yake ya Azam baada ya kufunga magoli 19 ya ligi kuu

Feisal amevuta milioni 90 kutoka kwenye klabu yake ya Azam baada ya kufunga magoli 19 ya ligi kuu

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kiungo huyo amechukua kiasi hicho cha pesa ni moja wapo ya kipengele cha mkataba wake na Azam fc kila msimu akifikisha magoli 10 na zaidi atakuwa akipata milioni 90.

kwahiyo tuseme Feisal katika miaka yote mitatu ya kimkataba atalamba milioni 270 kama atafikisha magoli hayo 10,ambapo kwa sasa amesalia na misimu miwili kwahiyo akifikisha magoli 10 ataondoka na milioni 180.

Vile vilabu vinavyomtaka Feisal hapo vipi wataweza kweli au waache tu watafute wachezaji wengine?

FEISAL-Salum-of-Azam-1.jpeg
 
Kama aliingia mkataba wa namna hiyo basi inatosha kusema Fei na timu yake walikuwa timamu.

Mpira ni mchezo wa muda mfupi lazima upige pesa vizuri, sio uzalendo uzalendo unakufa njaa, ukistaafu ni mwendo wa bakuli hata kama utaumwa ugonjwa wa laki.
 
Ni ushamba tu ila fei hajakosea kwa mustakabali wa maisha yake.

Kina totti, Gerrard, raul sio kwamba walikuwa loyal kwa timu zao kama sisi huku kina ngasa, hapana na mpunga mzuri walikuwa wanapata.
Kabisa mkuu
 
Kama aliingia mkataba wa namna hiyo basi inatosha kusema Fei na timu yake walikuwa timamu.

Mpira ni mchezo wa muda mfupi lazima upige pesa vizuri, sio uzalendo uzalendo unakufa njaa, ukistaafu ni mwendo wa bakuli hata kama utaumwa ugonjwa wa laki.
Hilo ni lakweli kabisa hala wana nzengo ndio wakwanza kumlaumu ya kuwa kachezea maisha yake wakati wa mikataba. Mungu ambariki asonge vyema ktk utendaji wake.
 
Kiungo huyo amechukua kiasi hicho cha pesa ni moja wapo ya kipengele cha mkataba wake na Azam fc kila msimu akifikisha magoli 10 na zaidi atakuwa akipata milioni 90.

kwahiyo tuseme Feisal katika miaka yote mitatu ya kimkataba atalamba milioni 270 kama atafikisha magoli hayo 10,ambapo kwa sasa amesalia na misimu miwili kwahiyo akifikisha magoli 10 ataondoka na milioni 180.

Vile vilabu vinavyomtaka Feisal hapo vipi wataweza kweli au waache tu watafute wachezaji wengine?View attachment 3008962
Usisahau kumshauri kununua viroba vya kutosha vya sukari na unga wa dona/sembe (kwa ajili ya kile kitoweo chake pendwa cha ugali + sukari), ili ikitokea siku akashawishiwa kuhamia timu nyingine; basi akose kisingizio.
 
Uamuzi wa kuhama timu haukuwa mbaya, ila wote waliomlaumu nikiwamo na mimi binafsi, ni njia aliyotumia kwani ndiyo iliyofanya watu wamchukie.
 
Hujanielewa Yani ikitokea amepata injury utashangaa bakuli linatembezwa wakati habari za kuvuna kama hivi
Ok, ila mkuu tukumbuke ukishakuwa hospitali inamaana huna uwezo wa kufanya kazi na hapo hapo unatakiwa ulipe bili za hospitali.
 
Back
Top Bottom