Feisal anatufundisha Moyo wa Mtu kichaka

Aende tu...

Aliondoka Lunyamila Yanga ije kuwa Feisal...
 
Said ana upuuzi fulani asee!! Nimeanza kumdharau kabisa.. ukanjanja unataka kuwa mwingi kwenye mambo yanayohitaji taratibu.
 
Kama feisal hana impact yoyote kwa yanga toka alipoaga kwanini mnaendelea kumng'ang'ania? Si mumuache akatafute maisha sehemu nyingine!
Mshauri afuate utaratibu, na pia ajitahidi kuwa muungawana. Yanga imemsitiri!

Simba ilimpotezea kumsaini. Azam ndiyo kwanza hawakuwahi hata kumuona kama ni mchezaji wa kumshajili! Ilimsajili, na baadaue akaboreshewa mkataba wake mpaka 2024!

Katika mazingira ya kawaida kabisa, Dogo alitakiwa kukaa mezani na Yanga kabla ya kufanya hicho alichokifanya. Yanga haina nongwa na mchezaji yeyote yule! Na ndiyo maana hata wakina Msuva walichezq kwa mafanikio, na baadaye wakaondoka.

Mtu kama Mrisho Ngasa, amecheza Yanga, akaondoka! Akarudi! Akaondoka tena!! Yaani mpaka dakika za mwisho anaachwa, tayari alishakuwa mwanajumuiya wa klabu ya Yanga.
 
Unachoshangaa hivyo nini?

Wanaachana watu waliokuwa wanalambana denda 24hrs/7, tena jamaa ukwasi umemwenea, kila akitakacho anapatiwa, sembuse mtu anayetafuta maisha yake ambaye mwisho wa siku anataka aoneshe kumbukumbu ya mateke aliyokuwa anapigwa viwanjani!!

Dogo kiu na Yanga imeshakatika.
 
Kama feisal hana impact yoyote kwa yanga toka alipoaga kwanini mnaendelea kumng'ang'ania? Si mumuache akatafute maisha sehemu nyingine!
unataka aondoke bure? hujui klabu zinategenea wachezaji kuuzwa?
 
Mkuu hapa wasipokuelewa, ni basi tu kwa kuwa kauli ya Haji Manara inaakisi ukweli kule Utopoloninyo.
 
Wacha bwanaa. Nyie si ndiyo mulimficha Ngasa na kumshauri azime simu wakati watu walikuja na mapesa yao ili wamsajili (nadhani viongozi wa timu mojawapo toka Sudan kama sikosei). Hamuwatakii mema au mafanikio wachezaji wenu. Mmemwachia Ngasa akiwa amekomaa kama bamia, kaenda South mpira umeisha, hakuchukuwa round huyu akarudi kucheza mpaka Ndanda. Kudadadek.
 
Ishu ya Ngasa ina utofauti kidogo na hii ya Feisal. Ngasa alikuwa ni mtoto wa mjini. Ilikuwa ni ngumu kumpeleka Sudan, halafu aache kula bata katika Jiji la Makamba

Alikuwa na uwezo wa kwenda kucheza Sudan. Ila hata yeye mwenyewe hakuwa na mzuka wa kwenda. Kwa Fei Toto, ni tofauti. Yeye ameamua kutukimbia, katika kipindi ambacho angeweza kutumia njia ya kiungwana ya kukaa na waajiri wake.
 
Mkuu umenena vyema. Feisal ana mengi sana ya kujifunza. Huo umaarufu wa Feisal ni matokeo ya kazi ya branding iliyo fanywa na Yanga. Yanga ndio wame mbrand Feisal. Yeye anafikiri ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wakati ukubwa wa jina lake ni nothing but branding. Yanga watamsahau Feisal ndani ya muda mfupi sana.

N.b,: nilicho jifunza ni kwamba Yanga ni brand ambassador wazuri sana
 
Tunaishi kwenye dunia iliyojaa USALITI Hilo nalo mjaribu kulifikiria,,,dogo anapambania ugali wake muacheni,,,namshukuru sana maana katoa funzo zuri
 
Ila Ngasa Ni bonge la kenge aisee yaani aliitema milioni 300 za wasudani ili achezee utopolo leo hii hata hela ya kulipia kuingia uwanjani hana na utopolo hawamkumbuki.
 
Ila nyinyi utopolo ni wachawi yaani mnamtemesha kijana wa watu milion 300 alafu leo hata hela ya kiingilio uwanjani anakosa ?
 
Umeandika ukweli mtupu hata luc eyamel aliyasema haya mkaja mkalia lia kawatusi wakati aliwaeleza ukweli
 
BInaadamu ni viumbe wanafiki sana, usiamini kabisa matendo yake ya usoni, mengi hua ya kuektia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…