Feisal "Feitoto" anachakujifunza kutoka kwa Carlinhos.

Abby Newton

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2017
Posts
1,252
Reaction score
2,253
Niseme tu kwa mara ya kwanza nimemuona Carlinhos akichezeshwa nafasi sahihi anayoimudu na aliitendea haki haswaa! Nadhani makocha waliopita hawakuliona hilo na hii ndio faida na hasara ya kubadilisha makocha. Kuna wa kunufaika na wa kuumia. Kufa kufaana.

Yanga ina mapungufu mengi lakini kukosa kiungo laini,mwenye akili, kasi, na uharaka wa maamuzi ndio vimekuwa vikiigharimu sana timu. Feitoto pamoja na uwezo wake wa kumiliki mpira na kukaba anatatizo la kupiga " Square pass" nyingi, anakosa sifa tajwa hapo juu.

Carlinhos aliimudu vilivyo nafasi ya kiungo namba 8, alimfundisha Feitoto nini maana ya kiungo mshambuliaji. Carlinhos anamacho, anaongozwa na akili,"He has an amazing passing accuracy" Ni nadra mno kumuona akipiga pasi mkaa, lakini pia ni"attacking minded"Mbele kwa mbele!

Endapo Yanga ingekuwa na "quality players" wa kiwango cha Carlinhos basi si ajabu Yanga angeshinda zaidi ya goli 3. Tatizo Mipira inapotea sana eneo la mbele, nidhamu ya kuutunza mpira si ya kutosha.

Kwa mechi ya Yanga vs Biashara kwangu Carlinhos ni "Man of the Match". What a player!

Natamani kumuona Carlinhos uwanjani mara nyingi zaidi kuanzia sasa.
 
Fei toto anatakiwa japo aendelezwe kielimu pia itamsaidia sana kujisimamia kama Carlinhos
 
Well Well, Carlos jana kauwasha sana.... mzenji ana chakujifunza pale
 
Kwani na ww ni mchambuzi au ume copy & paste kutoka kwa wachambuzi uchwara maana hawaishiwi vihoja
 
Performance may temporary but class is permanent. Carlinhos anajua tuache ushabiki maandazi
Aliemleta Carlinhos pale Yanga muda huu alitakiwa awe ameshawekwa ndani na takukuru"takukuru ng'ata"
 
Fei toto ni mchezaji wa kawaida sana, sifa anazopewa na anachofanya uwanjani huwa ni vitu viwili tofauti. Fei toto ni miongoni mwa wachezaji wa kuwaacha msimu huu, hatuwezi kwenda kimataifa na kiungo kama feitoto.
 
Fei toto ni mchezaji wa kawaida sana, sifa anazopewa na anachofanya uwanjani huwa ni vitu viwili tofauti. Fei toto ni miongoni mwa wachezaji wa kuwaacha msimu huu, hatuwezi kwenda kimataifa na kiungo kama feitoto.
Nakubaliana na wewe 100%, nasiongelei kwa leo tu nimekuwa nawaambia sana marafiki zangu ni mchezaji mzuri sio kama sifa anazopewa wa kawaida sana bahati pekee aliyonayo ule muonekano anapendeka ila kama atajiona ana safari ndefu na kutaka kujifunza atakuwa vizuri asiwe anasikia wapambe au magezeti uchwara jina la Toto linambeba
 
Kalinyo 'tepetepe' nami nakubali kweli ni garasa.....Ngoja tuone msimu ukipindua kama atabakizwa kwa watakaotimuliwa
 
Me jamaa yangu kila nikimwambia aniambie mechi yoyote ambayo Fei toto amewaka huwa ananiambia mechi ya Zanzibar na Tanzania basi lakini cha kushangaza bado anamuona mzuri, hapo ndio nikajua Yanga tuna safari ndefu.

Yanga hata leo wakicheza huwa namuona Tunombe Mukoko akifanya kazi kubwa ya kuchezesha timu na kuzuia huku Fei akiwa mzururaji tu uwanjani. Mukoko anafanya kazi kubwa sana akicheza na Fei Toto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…