Leo nimepata fursa ya kushuhudia huyu Kijana akicheza dakika zake 13 hapa Misri.
Kwa jicho langu la kiufundi huyu dogo ili acheze vizuri anahitaji hamasa sana hasa kutoka kwa mashabiki. Pia ni aina ya wachezaji wanaopenda kuzungumzwa ili afanye vyema kiwanjani.
Huyu dogo kamwe hatoweza kurudi katka ubora wake hata acheze timu yeyote ile hapa Afrika, labda akipata fursa ya kicheza mpira nje ya nchi ndipo atapata fursa ya kunolewa upya.
Yaani ni aina ya wachezaji kama Chama. Ili afanye vyema ni lazima mashabiki na waandishi wa habari wamsifie na kumzungumza kila wakati.
Licha. Ya fitness routine alizokuwa akifanya kipindi hayuko kambini na timu yake Yanga SC, bado anaonekana kuna kitu anakosa.
Unaweza ukamsaidia arudishe fitness yake ila ni ngumu saana kurudisha psychology yake ktk njia sahihi.
Dogo keshapotea.
Hata national team call up ilikuwa ni kwasabbu ya yule mpemba morroco aliyependekeza jina lake kwasababu za kiuzanzibar tu...Hakuna kocha mwenye leseni iliyo shiba anaweza muita feisal.
Kipaji kimepotea, ila kama taifa yatupasa tushukuru Mungu kwa kutupatiaMudathir Yahya.