Feisal salumu chutama na kuomba radhi kwa wana Yanga na viongozi wote, hakika utapotelea kusikojulikana

Feisal salumu chutama na kuomba radhi kwa wana Yanga na viongozi wote, hakika utapotelea kusikojulikana

Salary kidogo na bado awapigie magoti? Kichaa
 
Feisal amewekwa sehemu na watasha anakula marupurupu taratiibu...
Team za bongo kwa kukomoana,Subiri mkataba wake uishe ndio uamini,feisal atabaki dar...
Mpaka 2024! Bila shaka itamchukua muda wa kutosha tu kurudi kwenye kiwango chake cha awali.
 
Unapokosea siyo vibaya kuomba radhi na maisha mengine yaendelee huku mkono unakwenda kinywani, bila kujali makelele ya wafua vyuma.

Ndiyoooo, nimemuona Feisal wa Taifa Stars ni tofauti kabisa na Feisali kijana pendwa wa kocha Nabi.

Hakika kama Feisal akiendelea kuvimba huko mafichoni, kitakachotokea hata wale waliomjaza upepo watamkimbia na kutokomea kusikojulikana.

Najiuliza mpaka sasa Feisal anafanya mazoezi gani? Je, ni mazoezi stahili ili kujiweka fiti inavyotakiwa?

Nalengwa na machozi kwa kijana fundi, kijana mwenye talanta kupotea kwenye kiza kinene kwa sababu ya siasa za mpira wetu wa Kitanzania hasa hawa mapacha wa Simba na Yanga.

Mliomjaza upepo Feisali, tunaomba mumshauri arudi kuomba radhi ili asipoteze talanta yake ya football, kwa kweli alikaa miezi miwili bila mechi yoyote kaja kuonekana Taifa Stars, bwana mdogo kiwango kimeshuka.

Feisal asiposhituka mapema, namuona kabisa Simba, Azam na Yanga zikimkataa na kukimbilia Ruvu, mtibwa na nk.
Ugali sukari
 
Feisal amewekwa sehemu na watasha anakula marupurupu taratiibu...
Team za bongo kwa kukomoana,Subiri mkataba wake uishe ndio uamini,feisal atabaki dar...
huo mkataba unaishaje? huyu dogo hatacheza tena mpira tupo hapa
 
huo mkataba unaishaje? huyu dogo hatacheza tena mpira tupo hapa
Kama anaona bora kupotea kuliko kurudi Yanga yeye binafsi ndo anajua lililomkuta huko.
Mtu kama ww ikitokea akacheza utaumia ila asipocheza tena hakuna utakaloongeza.
 
Fei kasema wazi kabisa kwamba hawataki UTO.
 
Kama anaona bora kupotea kuliko kurudi Yanga yeye binafsi ndo anajua lililomkuta huko.
Mtu kama ww ikitokea akacheza utaumia ila asipocheza tena hakuna utakaloongeza.
Wewe ni sawa na shetani unajifanya unampenda kumbe unafurahia anguko lake
 
Namuona anavyokula mshahara wake bila jasho...

tena mimi ningekuwa huko morogoro vijijini na ATM card yangu kulima matikiti kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba

Kaka mshahara alilipwa kwa miezi 3 tu sasa iv apewi mshahara wala malupulupu kwa maana ni mtoro kazin!
 
Back
Top Bottom