Feisal salumu utakapoitikia wito wa taifa stars utakua umevunja msimamo wako wakutokua mchezaji halali wa yanga

Na ataonekana wazi utoto ndiyo unao msumbua. Aliyependekeza kuitwa kwa huyu dogo, anatakiwa kupewa pongezi.

Maana ametegwa patamu kweli kweli. Maana akitii wito, amejiingiza kwenye mtego dhidi ya timu yake! Asipoitikia wito, moja kwa moja ataonekana ni mtovu wa nidhamu kwa timu yake ya Taifa!

Time will tell.
 
Huna akili, unafungua nyuzi kila saa zisizo na kichwa wala miguu
Kuna mtu aliyekuzuia na wewe kufungua hizo nyuzi kila saa?

Kama ukiona unachukizwa sana, muweke tu kwenye ignore list yako.

Na kuanzia hapo, hutaziona hizo nyuzi zake za kila saa na zisizo na kichwa wala miguu.
 
Hapo kaitwa, akienda na akaperform mada zitafunguliwa za kutosha. Kuna mashabiki wanachotaka kuona ni Fei anapotea kimpira kabisa na wanajiandaa na hilo.
 
Hapo kaitwa, akienda na akaperform mada zitafunguliwa za kutosha. Kuna mashabiki wanachotaka kuona ni Fei anapotea kimpira kabisa na wanajiandaa na hilo.
Sana sana simba sc maana wao ndiyo wameleta figisu mpaka akaondoka yanga

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: Tsh
Na akiitikia wito aje kutueleza ameitikia Kama mchezaji wa timu gani.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Haina madhara kwa dogo Fei. Aende tu Taifa Stars. Japo atamkuta Kaze kajaa pale! Akizingua na hapa arudi tu JKU!
 
Haina madhara kwa dogo Fei. Aende tu Taifa Stars. Japo atamkuta Kaze pale! Akizingua na hapa arudi tu JKU!
Naona dogo mmeamua kumuweka mtu kati. Wenye mamlaka za juu wameamua kumshughulikia.
 
Nadhani ni muhimu kumsaidia Fei kujua tofauti ya uhuni na sheria
Mnachanganya mambo. Focus ingekuwa kujenga kikosi cha ushindi siyo kuita watu ili tu kuwatega
 
Mnachanganya mambo. Focus ingekuwa kujenga kikosi cha ushindi siyo kuita watu ili tu kuwatega
Na ametegwa sasa! Tuone atajiunga na timu ya Taifa akitokea Yanga, au atapuuzia wito ili kuudhihirisha utoto wake.
 
Na ametegwa sasa! Tuone atajiunga na timu ya Taifa akitokea Yanga, au atapuuzia wito ili kuudhihirisha utoto wake.
Timu inayojinasibu kuwa ni kubwa haihangaiki hivyo. Mnaendelea kumlipa mfanyakazi hewa kwa kujisifu kabisa.
 
Timu inayojinasibu kuwa ni kubwa haihangaiki hivyo. Mnaendelea kumlipa mfanyakazi hewa kwa kujisifu kabisa.
Yanga inatimiza wajibu wake kwa mchezaji, na pia inaheshimu mkataba iliyoingia na huyo mchezaji.

Hivyo sioni kama kuna tatizo kwa upande wa timu, isipokuwa kwa huyo mchezaji siku za usoni. Maana atalazimika kuutapika huo mshahara anaolipwa kwa sasa.
 
Kuwarudishia pesa yenu siyo shida, inawezekana hata haigusi au anaizungusha tu sasa hivi 🤣😂🤣 Kama aliweza kuwapa zaidi ya milioni 100 atashindwa kuwarudishia milioni 20 sijui ambazo mlimtumia wenyewe?
 
Hivi zile milioni 100 alizoweka kwenye akaunti ya Yanga ili kuvunja mkataba wake, alizipata wapi kama mchezaji alikuwa anashindia ugali na sukari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…