Mchezaji mkubwa anaonekana katika mechi kubwa, Feisal hakucheza vizuri, kama baadhi ya wachezaji wengi walio cheza Chini ya kiwango.
Feisal alitakiwa aonyeshe yeye ndiye namba 10 wa timu yetu ya Taifa lakini kilichotokea ni kama hakuwepo.
Feisal anajua mpira ila hana nguvu, eneo analo cheza linahitaji ku ujua mpira na uwe na Nguvu za kupambana kwakua yeye ndiye kitovu Cha mashambulizi ya timu.
Walio bahatika kumuona Yusufu Macho (Muso) wataelewa naongea Nini.
Macho alikua namba 10 anaujua mpira, anapiga mashuti anachezeaha timu, ana Nguvu.
Alikua ni mchezaji wa kwanza Mtanzania aliye kwenda kukipiga Jomo cosmos ya South Afrika baada ya coach Jomo Sono raia wa South ku ukubali mziki wa Yusufu Macho Mechi na south Africa
Zile mechi ITV walikua wakizionyesha, wahusika pale Tff waongee na ITV wapate video wamuone Yusufu Macho alikua mwamba wa namna Gani katika nafasi ya namba 8 au 10 wajifunze kitu.