Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Mbona kijana wetu hana shida tena ya maisha!! Kwa sasa analipwa mshahara wa milioni 16, badala ya ule mshahara kiduchu wa milioni 4! Na uliomfanya ashindie ugali na sukari!Hapa Tanzania wachezaji wanapitia wakati mgumu ambao sio wageni na waeleza wale wachezaji wa ndani. Timu mbili ambazo zinaweza kukupa mashavu na madili makubwa ni Simba na Yanga, ila hizo hizo zinaweza kukuweka gizani.
Feisal kwa sasa kama hakuna anayemfatilia ukilinganisha kipindi yupo Yanga na dili za matangazo. Kuna msemo usemwao; "Kila penye mafanikio washauri wa kila aina wanaongezeka."
Ili linaweza kuwa ndio lililomtoa kwenye njia. Tanzania sio Uingereza sababu kwenye vilabu vilivyo na nguvu hapa ni viwili tu.
Ukitoka hapo hakuna atakayekusikia wala kuwa na muda na wewe upande wa mashabiki mpaka madili ya maana.
Ugali kwa sukari.
Kijana kanunuliwa nyumba, kapewa gari kali! Akitaka ice cream za Azam anapewa bure!! Eeeh!! Kijana amekosa nini!! Kwa sasa analea kitambi chake , kama aenzake akina Sopu, nk!! Baada ya hapo, atahamia zake simba! Timu ya ndoto yake!!!