Mm ningekuwa shabiki wa Yanga nisingekuwa upande wa viongozi na kichaka chao cha kufuata taratibu. Ningewahoji kwa kutokuthamini mchango wa kijana mzawa.
Sawa Fei alisain mkataba kabla hatujakiona hichi kiwango ndo maana mkataba ulikuwa wa thamani ndogo, ila baada ya kukiona kiwango kwann hatukuwa wa kwanza kumshawishi na mkataba wenye maslahi bora mpaka waje wengine kutoka nje?
Kuna harufu ya viongozi fulani fulani hapo kumnyonya Fei. Na tunajua akili za baadhi ya wabongo wakiwa wameshika mpini. Unaweza kuta Fei alishaomba sana tu wamwangalie ila zile roho fulani hivi zikasababisha wasijali na kuchukua hatua kwa wakati na sasa hivi watavaa ukondoo chini ya kivuli cha taratibu hazikufuatwa.
WANAYANGA WATAFUTE CLIP ZA FEI AKIIPIGANIA YANGA HALAFU WAJIULIZE, YULE ANAFANANA NA MCHEZAJI ALIYEICHUKIA YANGA NA KUTAKA ATOROKE ISIPATE CHOCHOTE? SIKU AKIWA ANASTAAFU ANAWEZA ONGEA YALIYOMKUTA.
KWA SASA ATATULIA KWANI HAKUNA MCHEZAJI MKUBWA KULIKO CLUB NA NI HATARI KUZUNGUMZIA CLUB ULIYOTOKA VIBAYA WAKATI BADO UNAHITAJI CLUB NYINGINE IKUSAJILI.