'Feitoto' punguza huna thamani ya Shilingi Bilioni Moja za Kitanzania kwa Timu inayokutaka sawa?

'Feitoto' punguza huna thamani ya Shilingi Bilioni Moja za Kitanzania kwa Timu inayokutaka sawa?

Bora hata ungemsema mdadhir ungeeleweka
Labda kama hujawahi kucheza mpira ila hakuna midfield wa bongo ambae hajafika miaka 30 hivi sasa ambae hajawahi kutamani kucheza kiungo kama anavyocheza Sureboy.
 
sure boy ni better than Fei. sure boy ni umri tu ila bonge moja ya mchezaji. Fei at his age awezi toboa
Kwanini tutumie hisia kujadili uhalisia? Weka hapa takwimu za Sureboy at his age. Ubora ni namba sio kupayuka tu. Tutembee kwa mifano halisi onesha Sureboy ali offer vitu gani katika kipindi chake ambacho Feisal hajaweza ku offer hadi sasa. Tuongee kimpira sio kimipasho. Njoo na data
 
Labda kama hujawahi kucheza mpira ila hakuna midfield wa bongo ambae hajafika miaka 30 hivi sasa ambae hajawahi kutamani kucheza kiungo kama anavyocheza Sureboy.
Sureboy anayeongelewa ni yupi kwanza? Ni yule alikuwa anacheza sigara kisha Yanga? Au ni huyu mtoto wake aliyetoka Azam kisha Yanga? Kama ni huyu wa sasa, basi haya maoni ni kwavile hachezei Yanga hivyo ni wivu, roho za kuachwa ndizo zinazotoa maoni kwenye hili.
 
UKiondoa wachezaji wa kigeni hakuna kiungo wa ushambuliaji bora nchi hii kumzidi Feisal Salum Abdala, Fei Toto

Sijazungumzia kuhusu kudeserve 1B au la ila ninachojua kwa namna yoyote ile kwa sasa yeye ndio mchezaji ghali zaidi wa kizawa katika ligi yetu huku akizidiwa thamani na wachezaji wachache sana wa kigeni wasiozidi watano

Kwahiyo kama Fei hafiki 1B basi ni wazi hao viungo wengne wote unaowajua kwenye nchii hii hawafiki hata 300m.

NB: Thamani ya 1B ni kiasi kilichowekwa na klabu yake ya Azam kwenye "release clause" yake na sio Fei mwenyewe ukumbuke Fei ana mkataba na azam hivyo ni klabu ndio inataja thamani yake kwa wanaomhitaji na sio mchezaji mwemyewe
 
Feitoto kama asset anayo thamani ya zaidi ya hiyo bilioni moja. Ila Feitoto kama mcheza mpira hajafikisha vigezo vya kuwa na thamani hiyo.
 
Back
Top Bottom