Uchaguzi 2020 Felister Njau: Tulikamata mabegi matano ya kura za CCM ktk Uchaguzi Mkuu 2020

Mkuu nakushukuru kwa kuliona hilo. Ndugai alitaka kuwahadaa nchi Wahisani wanaotoa fedha zao kwajili ya kukuza Demokrasia waendelee kufanya hivyo.

Wale covid-19 ndiyo iliyokuwa kete yake ya kwanza. Alitaka kuwaonyesha kuwa Bunge analoliongoza ni la Demokrasia tena kwa vitendo. Wakati huo huo akiwaaminisha Nchi Wahisani kuwa Chama Kikuu cha Upinzani hakina Demokrasia imetawaliwa na mfumo Dume. Atawaambia kuwa wale Wabunge wa Viti Maalum walipendekezwa na Chama ila M/K wao akawakatalia. Yeye kama Spika akawapigania. Tatizo linakuja wapi? Katiba ya Tanzania iko wazi huwezi kupata nafasi yeyote ya Kisiasa bila kudhaminiwa na chama cha siasa chenye usajili. Kwa hapa nchini tu Ndugai ameshindwa kutetea hoja yake Kisheria. Kaamua kutumia ubabe na madaraka yake. Limebuma.

Sasa kete ya pili ni kuwaondoa Mjenggoni wale Covid-19 na kuwarehesha kwenye chama chao cha awali wakamalizane. Kwa vyo vyote vile maamuzi ya chama yako wazi. Walishatimuliwa hivyo wataakimbilia Mahakamani. Mahakama itaweka zuio la muda. Hivyo kuamuru chama kuwarejeshea uwanachama wao hadi kesi yao ya msingi itakapisikilizwa na kutolewa maamuzi. Wale covid-19 watarudi Mjengoni kwa amri ya Mahakama.

Ndugai atarudi kwa wale Wahisani na kuwaambia mumeona Mahakama imeona vile Wabunge wanawake wanavyonyanyaswa hivyo imeamua kulishughulikia suala lile la Kidemokrasia Kisheria Mahakamani. Hivyo mtupatie mpunga. Naamini nalo litabuma.

Mwisho nitoe rai kwa Wapenda Demokrasia ya kweli na Wenye Mapenzi mema na Nchi yetu tuendelee kuwaombea afya njema Wapambanaji wetu walioko Nje ya Nchi. Mh Lissu na Mh Lema kwa uchache na Wengineo yaani Makamanda Wetu wote.
 
Mbona nimesikia wapinzani hamfuatilii kikao cha CCM Kinachoendelea Dodoma.
 
Kwa vyo vyote vile maamuzi ya chama yako wazi. Walishatimuliwa hivyo wataakimbilia Mahakamani. Mahakama itaweka zuio la muda.
Najua ubovu wa mihimili hii miwili Mahakama na Bunge; lakini sikujua kwamba pamoja na ubovu ule "Mahakama wanaweza kuamuru wanachama waliofukuzwa ndani ya chama warudishwe"?
Hili sikulijua.
Mwisho nitoe rai kwa Wapenda Demokrasia ya kweli na Wenye Mapenzi mema na Nchi yetu tuendelee kuwaombea afya njema Wapambanaji wetu walioko Nje ya Nchi. Mh Lissu na Mh Lema kwa uchache na Wengineo yaani Makamanda Wetu wote.
Waliomo nchini wanazihitaji sana hizo sala, pengine zaidi ya wale walio nje.

Yote kwa yote mkuu 'halaiser', ninakubaliana na haya uliyoandika hapa.

Tatizo pekee ninaloona ni kutegemea hao wenye pesa anazotafuta Ndungai. Hawa sio watu wa kuwaamini hata kidogo. Wana maslahi yao wanayoyaweka mbele ya mahitaji ya wananchi wetu. Hawa ni rahisi sana kuuza mahitaji ya wananchi wetu ili mradi tu ya kwao yafanikiwe.

Mfano mzuri wa hivi karibuni ni hao wa EU, ambao sasa wanaonekana kukubali uchaguzi uliochafuliwa na kutazama maslahi yao.

Tuachane na kuwategemea hawa wazungu kwa lolote. Matatizo yetu tutayatatua sisi wenyewe kwa njia zetu wenyewe.
 
Big No kwa huu mtazamo wako. Sheria na taratibu walizojiwekea kwenye taasisi yao lazima ziheshimiwe na zifuatwe na kila mmoja, kitendo cha wao kupuuza maazimio ya KK ya chama chao na kukimbilia bungeni tena bila kufuata taratibu husika hakiwezi kuvumiliwa eti tu kwasababu wanaonekana wako "active" ndani ya bunge, hao lazima waadhibiwe kwa ukaidi walioufanya bila kujali nini wanakisema au kukifanya sasa hivi wakiwa bungeni, full stop.
 
Kuvumilia njaa ni kazi kubwa sana, hata wanaume wanashindwa.
Sitaki ugomvi na jirani yangu kijijini, lakini Mbowe anaweza kukushauri kwa suala la kuvumilia njaa.
Lakini hujaambiwa upambane na njaa yako kwa hila, pambana kwa halali ata dini yetu inatufundisha hivyo.

Ni jambo la aibu sana kwa hawa tunaowaita Covid-19 kwa status waliyotokana nayo na walivyomalizia, ni wazi wamekata tamaa na kudhani nusura yao ni kurudi bungeni in anyway., siku hazigandi miaka mitano itaisha. Life is always there
 
Nitakataa vipi haya uliyoandika hapa mkuu wangu 'denooJ'.

Kukataa taratibu za chama au taasisi yoyote ni sawa na kukubali yanayofanywa na utawala huu uliopo madarakani, ambao kwao taratibu, sheria au hata Katiba vyote haviwazuii kufanya wayatakayo.

Hayo niliyoyasema hapo juu na wewe kuyaelewa hivyo ni kwamba tu'assume' kuwa ni mpango kabambe wa chama, CHADEMA kuwatoa kwenye mstari wachafuzi wa uchaguzi kwa kutumia mbinu zile zile chafu wanazozitumia watawala.

Ni vigumu kuamini kwamba hivyo ndivyo, lakini kama kweli kuna mpango wa aina hiyo, basi huko CHADEMA watakuwepo watu makini sana.
Yaani kutumia mchezo mchafu kupiku mchezo mchafu waliofanyiwa wao!

Ndio maana nikasema, kama hii ni kweli, basi hao wabunge hawana uhai bungeni, lakini watakuwa wameonyesha ujuzi wa hali ya juu sana.

Kumbuka, huu mpango hauwezi kuwa wa wabunge wenyewe, yaani COVID-19, bali utakuwa ni mkakati wa chama, wao watakuwa ni watekelezaji tu wa maagizo ya mipango ya chama.

Ikibainika hapo baadae kwamba hii ni mbinu iliyobuniwa na CHADEMA, ya nini kuendelea kushikilia msimamo wa kuwalaumu wanaoutekeleza kwa heshima kubwa kwa chama chao?

This may be too far away fetched, but it is possible.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…