Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
FEMINA HIP mmepotelea wapi ndugu zetu? Zamani mlitoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya magonjwa ya ngono, mimba za utotoni nakadhalika. Vijana wengi tulivutiwa sana na Magazine za Femina Hip kwasababu tulifahamu njia zote mbaya za kutuingiza kwenye vishawishi vibaya
Hakika tulielimika sana ikiwemo mimi binafsi niliyeelimika. Sijajua mpaka sasa nini kiliwasibu sijapata majibu mliondoka hewani ghafla
Hivi sasa tuna wimbi kubwa la vijana kujiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja, limeshakuwa ni tatizo kubwa sana
Tafadhali jitahidini kurudi hewani muwaongoze vijana wetu na kuwapa mbinu za kujilinda na janga hili
Chague Channels mtakazofanya nazo kazi, zipo nyingi kuna Wasafi Tv, Crown Tv, Clouds Tv, EATV, ETV, TBC, na nyinginezo.