Feni kwa mtoto

gjosem

Member
Joined
Sep 23, 2017
Posts
10
Reaction score
5
Habari za majukumu wana jf mimi nina mtoto wa miezi 7 na nusu na mazingira ninayoishi yanajoto sana kiasi kwamba hata nikifungua madirishi bado joto linakuwa juu kiasi kwamba mtoto anapata tabu sana wakati wa kulala iwe mchana au usiku na hutokwa jasho sana kwahiyo naomba ushauli wenu kama ni salama kwa afya yake kama nikimuwashia feni maana huwa naogopa sana kuwasha feni.
 
Fan haina shida kwa watoto wadogo... Meaning haina direct effect.

Ila kutokana mazingira ya kiafrika hususani kitanzania ambapo vumbi inakuwepo mpaka ndani unashaurikwa kutotumia fan kwa sababu feni inapozunguka kama chumba kina vumbi inafanya ile vumbi iwe ina zunguka mule ndani na mtoto anakuwa anaivuta ile hewa yenye vumbi na uwezo wa kuitoa vumbi kutoka kwenye mfumo wa hewa kwa mtoto bado haujakomaa kama mtu mzima ambavyo akiona vumbi imeingia anaweza kukohoa.

So kama unauhakika na usafi wa mazingira mtoto anapoishi basi unaruhusiwa kabisa kutumia Fan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…