Ferooz: Rais Mkapa hakuninunulia gari

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Msanii Ferooz

Msanii Ferooz ambaye alikuwa kwenye kundi la Daz Nundaz ambaye amewahi kufanya vyema na ngoma kibao kali ikiwepo 'Starehe' amefunguka na kusema Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa hajawahi kumnunulia gari kama watu wanavyodhani.

Ferooz amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kudai kuwa mtaani kulikuwa na maneno kuwa amenunuliwa gari aina ya Jeep na Rais jambo ambalo si kweli.

"Mimi nashukuru Mungu Rais Mkapa alizungumzia kwenye hotuba yake kuwa nimefanya jambo zuri kupitia wimbo wangu 'Starehe' na akasema nina stahili zawadi kwa kazi ile, hivyo katika kipindi hicho hicho mimi nilikuwa ndiyo nilikwenda kununua ile gari Jeep, kwa hiyo ile gari nilinunua kwa pesa zangu za muziki nilikwenda kununua Dubai na kuiingiza nchini mwenyewe, hata hiyo zawadi ambayo Rais alisema nastahili kupata sikuwahi pata" alisema Ferooz.

Mbali na hilo Ferooz anasema gari hilo baadaye alikuja kuliuza kwa kuwa aliona tayari limepitwa na wakati

"Ile Jeep kwa kifupi baadaye nilikuja kuiza maana ingekuwepo mpaka leo huenda ingekuwa banda la kuku, kwa hiyo niliiuza kama miaka kumi iliyopita huko" alisisitiza Ferooz

Mbali na hilo msanii huyo ameahidi kuwa sasa anajipanga kuja kivingine katika muziki na kuwataka mashabiki kutotilia manani maneno ambayo yapo mtaani na kusema watu wanakuwa wazushi kwa mambo ambayo hawayajui

Chanzo: EATV
 
Shukran kwa kulitolea maelezo Manaake hii taarifa hata kwetu huku ushetu ilisambaa vilivyo yakwamba ulipewa gari na Mh. Mkapa

Nawaheshimu sana wasanii wakongwe hapa Tanzania mlikitendea vyema kipindi chenu kwa nyimbo zenu nyingi zilizo na lundo la mafundisho katika Jamii na uhalisia haswa!!

Nyakati zinabadilika,heshima kwenu wakongwe!
 

Nyimbo za wasanii wakongwe hazijawahi kukinai kama hizi za akina sheta!

Pini kama mkasa wa boss, barua, wife, mtazamo, nikusadieje, vumilia and the list goes. Ubora na uthamani wake sio kushuka Leo wala kesho kwa mtu anaeujua muziki.

Muziki zamani, siku hizi ni utani,hakuna hata burudani wala madini, akili zao zote zipo sokoni.

sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.
 
Mkuu Lizarazu!
Za siku vipi mwanamalundi.

Ni hatari kizazi hiki muziki upo zaiidi kipesa-pesa na kingono-ngono.

Ukisiliza ngoma za wakongwe unapata vitu halisia na Maarifa.

Nyakati zinabadilika hatuna budi.

Kuna wimbo wa "wema wangu umeniponza" wa ferouz naupenda kweli kweli na wimbo wa "boss".

Lukagoal umemuona Jana...?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu!
Saizi kila Mtu anaweza kuwa msanii,Sasa ubora utatoka wapi..?

Hakika dunia imebadilika,wao pesa Kwanza!!
 
Huyu aende kwenye lebo ya Mhenga kutamsaidia kutoka. Kule wakiungana na Chidi Benz, Maunda Zoro, Hawa, Mnyama TID, Q Chillah, Ray C watafanya vizuri.
 
ahadi ni deni....angemkumbusha tu labda atatimiza ahadi yake.
 
Kwani Sheta anaimba!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Salama kabisa mwanamalundi mwenzangu.

Hiki kizazi cha muziki-pesa hakina la maana zaidi ya kufanya noise pollution, tunaskilizaga kwa bahati mbaya tukiwa kwenye mkusanyiko wa watu.

Lukaku sikumuangalia ila nimeona highlights jinsi mlivyo waadamisha city 2-0. Mko vizuri sana hongereni

sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.
 
Ndugu yangu!
Saizi kila Mtu anaweza kuwa msanii,Sasa ubora utatoka wapi..?

Hakika dunia imebadilika,wao pesa Kwanza!!
Hata mimi mwenyewe nampango wa kuingia studio maana nna ma freestyles mshenzi kibao tu ghetto. [emoji13] [emoji13]

sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…