Ferooz: Rais Mkapa hakuninunulia gari

Ferooz: Rais Mkapa hakuninunulia gari

Gari aliliuza kwa sababu lilikuwa linabugia wese Hatareee

Ova
 
View attachment 547472
Msanii Ferooz

Msanii Ferooz ambaye alikuwa kwenye kundi la Daz Nundaz ambaye amewahi kufanya vyema na ngoma kibao kali ikiwepo 'Starehe' amefunguka na kusema Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa hajawahi kumnunulia gari kama watu wanavyodhani.

Ferooz amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kudai kuwa mtaani kulikuwa na maneno kuwa amenunuliwa gari aina ya Jeep na Rais jambo ambalo si kweli.

"Mimi nashukuru Mungu Rais Mkapa alizungumzia kwenye hotuba yake kuwa nimefanya jambo zuri kupitia wimbo wangu 'Starehe' na akasema nina stahili zawadi kwa kazi ile, hivyo katika kipindi hicho hicho mimi nilikuwa ndiyo nilikwenda kununua ile gari Jeep, kwa hiyo ile gari nilinunua kwa pesa zangu za muziki nilikwenda kununua Dubai na kuiingiza nchini mwenyewe, hata hiyo zawadi ambayo Rais alisema nastahili kupata sikuwahi pata" alisema Ferooz.

Mbali na hilo Ferooz anasema gari hilo baadaye alikuja kuliuza kwa kuwa aliona tayari limepitwa na wakati

"Ile Jeep kwa kifupi baadaye nilikuja kuiza maana ingekuwepo mpaka leo huenda ingekuwa banda la kuku, kwa hiyo niliiuza kama miaka kumi iliyopita huko" alisisitiza Ferooz

Mbali na hilo msanii huyo ameahidi kuwa sasa anajipanga kuja kivingine katika muziki na kuwataka mashabiki kutotilia manani maneno ambayo yapo mtaani na kusema watu wanakuwa wazushi kwa mambo ambayo hawayajui

Chanzo: EATV
huyu hana chake tena,atafute shughuli ya kufanya ,muziki hauwezi.
 
Nyimbo za wasanii wakongwe hazijawahi kukinai kama hizi za akina sheta!

Pini kama mkasa wa boss, barua,wife,mtazamo,nikusadieje,vumilia and the list goes.... Ubora na uthamani wake sio kushuka Leo wala kesho kwa mtu anaeujua muziki.

Muziki zamani, siku hizi ni utani,hakuna hata burudani wala madini, akili zao zote zipo sokoni.

sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.
Mkuu huu wimbo wa Vumilia Naweza kuupata wapi?

Sent From Mhenga Aliyesema Hasomeshi Wazazi
 
"Nini mnataka mazee,Mafansi hawakujibu"
"Zamani wangejibu Rhymes,Leo imebaki aibu"

Nikki Mbishi-Nyakati
 
Back
Top Bottom