Festo Sanga: Rushwa imekithiri nchini, inaathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Jimbo la Makete (CCM), Festo Sanga, amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini hauwezi kufanyika kwa wakati iwapo tatizo la rushwa litaendelea kushamiri.

Kauli hiyo alitoa leo Jumanne, Februari 3, 2026 alipokuwa akichangia Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Muda wa Kati wa mwaka wa fedha 2026/27 hadi 2028/29.

Mbunge Sanga ameeleza kuwa rushwa imekuwa chanzo kikuu cha ongezeko la gharama za miradi ya maendeleo, huku Serikali ikilazimika kutumia fedha nyingi kulipa mikataba ambayo mara nyingi haitekelezwi kwa wakati.

"Hatuwezi kutekeleza miradi hii ipasavyo endapo rushwa itaendelea kushamiri katika taifa letu. Mikataba mingi inagharimu fedha nyingi, na Serikali inalipa gharama kubwa kwa miradi ambayo imegeuka kuwa mzigo kutokana na kushindwa kutekelezwa kwa wakati, hali inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na rushwa," amesema Sanga.

Mbunge huyo amesisitiza pia umuhimu wa kuimarisha Uwajibikaji na kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inawanufaisha Wananchi kama ilivyokusudiwa.

​
 
Hivi kumbe watu walikuwa wamelala na hivi sasa ndiyo wanatoka ndotoni?
 
maneno matupu bila ushahidi ni porojo tu :HAhaa:
 
Asubiri kuhojiwa na takukuru huyu mwamba
 
Back
Top Bottom