jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Asante kwa fursa.Hii ukiwa unakodisha Mbudya unapiga pesa nzuri, pia kwa wale wanaopenda kununua Toyota Ist na kumpa dereva wa Uber ni bora 14million uchukue boti yenye engine uwe unakodisha kwa wavuvi.
Kwa Dar kukodi boti ni elfu 15,engine 15, nyavu 15 jumla siku moja unapata elfu 45 wavuvi wapate samaki wasipate asubuhi lazima wakupe elfu 45. Ukiweka kukodisha watalii hakuna presha kwa chombo,engine na mfanyakazi kwa siku hukosi elfu 50. Ukikata na comprehensive Insurance mwaka mzima haizidi laki 2.
Boti haina risk ya kugongwa,kupigwa pasi, madeni ya traffic, hiyo bima itakulinda incase engine imeibiwa maana walipo watu weusi si salama kujihamini.Moto au kuzama utalipwa pasi na shaka.
#MaendeleoHayanaChama