Fibre internet ina kasi, haina kikomo, bei chee, unawekewa bure. Wateja tupo, tunawaomba mpanue huduma zenu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kwa hii kasi ya mabadiliko ya vifurushi, tujipange isaikolojia, huenda tukaingia 2022 GB1 ikiwa inauzwa elf 2,500 sawa na petrol.

Fibre internet ni internet inayoletwa kwako kwa njia ya waya na uutapewa bure vifaa vya kusambaza internet kwa njia ya wifi.

Gharama zao zinaendana kwa speed na sio vikomo vya gb kama tulivyozoea, Mfano kifurushi cha chini cha elfu 60 kwa mwezi huwa kina spidi ya kudownload MB 1 kwa sekunde, kifurushi cha elf 80 utaweza kudownload MB 2 kwa sekunde, n.k. hata ukidownload gb 20 kwa siku ni wewe tu, taangalia youtubr, netflix, n.k kwa kiwango cha juu bila mawazo ya GB.

Ni huduma ambayo inafaa mno kuwepo majumbani ama maofisini, adala ya kila mtu kujiunga kifurishi, mnaweza wote kutumia huduma ya fibre kwa njia ya wifi.

Kwa hapa kwetu huduma hizi zipo tu Dar na sehemu iliyopo Dar ni chache hususani za city centre ndio watakuvutia waya.

Kiukweli hatutendewi haki kwa haya mabando ya mitandao ya simu, Sio kwamba kusema tunashindwa kulipa ila ni kwamba internet yafaa kuwa hitaji la gharama nafuu, Ni muda muafaka wa makampuni ya fibre waanze kuwekeza kwenye upanuzi wa huduma zao kutufikia hata huku mikoani.
 
Tatizo wako city center huku kitaa huduma zao hazipo sijui kikwazo nini?
 
Duh,hii kitu ni nzuri Sana na hawa wengine wanajiitaga sijui zuku mara simbanet
 
Tanzania tulikuwa tunaongoza kwa kuwa na vifurushi bei chee vya simu, hii iliwakuwa inawapa wasi wasi
So kuna uwezekano nao fibre wakaongeza gharama kwasababu washajua hatuna pakutokea?
 
Tanzania tulikuwa tunaongoza kwa kuwa na vifurushi bei chee vya simu, hii iliwakuwa inawapa wasi wasi
Nikweli vifurushi vilikuwa Chee,serikali ilikuwa imejiongeza,wananchi wake waweze kupata elimu kupitia internet pia waweze kufanya biashara za mitandao zenye manufaa n.k ,lakini kinyume chake watu wakaitumia internet vibaya kama kurusha picha za utupu,kutukana viongozi,kupost picha za maafa na ushabiki mwingine usiofaa,mwisho wa siku serikali ikapandisha bei za vifurushi ili kuchuja wale watu wenye ujinga huo wasiweze kutumia internet.
 
Ujinga mtupu,sema Mataga hawanaga akili ya kujua internet Ni kila kitu kwny Maisha kwa Sasa hivi.
 
Nikweli vifurushi vilikuwa Chee,serikali ilikuwa imejiongeza,wananchi wake waweze kupata elimu kupitia internet pia waweze kufanya biashara za mitandao zenye manufaa n.k ,lakini kinyume chake watu wakaitumia internet vibaya kama kurusha picha za utupu,kutukana viongozi,kupost picha za maafa na ushabiki mwingine usiofaa,mwisho wa siku serikali ikapandisha bei za vifurushi ili kuchuja wale watu wenye ujinga huo wasiweze kutumia internet.
Mkuu,
Hizi ni akili zako???
 
Back
Top Bottom