Hapana.!
VPN ni kifupi cha maneno haya...Virtual Private Network.
Hii ina maana, ukishajiunga na internet yako (yaani ukiwa online katika kifaa chako eiza simu au kompyuta) unapata kitu kinachoitwa IP Address ambayo kimsingi inaonesha wapi kifaa chako kimeunganishwa na internet iyo (yaani ina ku'pin point)
Sasa kwa kuweka VPN inakupa address nyingine tofauti yaan kwa mfano VPN yako ni ya USA basi automatically mtu akiangalia upo wapi kwenye kifaa chako ndio itaonesha upo uko USA na si iyo excatly location uliyopo.
Nimefafanua kidogo kwa uelewa wangu, wengine wanakuja watajazia pale nilipoacha na kunikosoa pia inaruhusiwa.
Melvine.!