Fid q awaomba radhi wasafi asema alikuwa hajielewi na awezi kuwa kinyume na Clouds media

Fid q awaomba radhi wasafi asema alikuwa hajielewi na awezi kuwa kinyume na Clouds media

Fid Q angepata elimu kubwa angeweza kuwa mwanadiplomasia wa kuwapatanisha Israeli na Palestina. Jamaa kajaaliwa upeo mpana sana
 
Mara kwanza sikuamini kama Fid q kaongea hivi as long mwenyewe kakubali ni kweli alikosea kuwaita mafala ,japokuwa aliweka kimafumbo .Tatizo kubwa la wasanii wa Tanzania hawajiamini SUGU kipindi kile ana fight alionekana kama mtukutu na wasanii wakamtenga,Jide nae kajikakamumua mpaka wasanii wenzake wakamtenga lakini akafanikiwa kufanya mambo yake.

Mondi na WCB nao naona wameamua kujitegemea naona wasanii wenzao nao wanampiga vita.Siku zote hauwezi kuwa ww peke yako,ili uwe bora lazima upewe changamoto.Miaka ya nyuma kulikuwa na watu wanaanda matamasha makubwa kaletwa kanda bongoman,brenda fasie,vyone chakachaka,koffi olomide nk na yakafanyika matamasha makubwa.

Ila walivyokuja hawa CMG wakagundua ,kuna baadhi ya mikoa inakosa burudani na ndio maana wakaja na Fiesta na CMG .Kumbuka hata huko nyuma Radio kubwa zilikuwa Radio One na Radio free wakaja wao wakafanya mapinduzi,Hivyo hivyo nao WCB nao wameona fursa wanatakiwa waitumie na kweli wameitumia ,sioni kosa apo japo kuna watu eti wanasema hawana adabu.

Lakini ukitaka kujua fitina za CMG muulize Majizo(wengine Sugu,Jide),hamna mtu aliyekuwa kapigwa fitina tena fitina za kutatisha tamaa kama Majizo,bahati nzuri jamaa mpambanaji mpaka leo hii nae anatamasha lake la KOMAA CONCERT .Wasanii wanatakiwa kuwa kama service provider kwa haya matamasha na kuhusu ubora wa matamasha waachie waandaaji na si kuwa mashabiki kwani kwao haitawajenga kiuchumi,hivi vijembe vya mafumbo havitawasaidia wawachie waandaaji wao ndo wapigane vijembe.
Ndio ajifunze kutokuwa na upande , kwenye vita ya wakubwa
 
Namnukuu Farid Kubanda

@babutale PART 1: Nimeonelea si vibaya nikifungua hiki kigazeti changu na sentensi hii—-.> “ Keki ya taifa ni kubwa sana na ina vipande vingi vya kuwatosha wachakarikaji wote wenye kuistahiki “
Na kwakua Allah ndio mtoaji riziki, mimi kama mimi sina hayo mamlaka au hata hiyo roho mbaya ya kutamani wachakarikaji wenzangu mkwame ktk harakati zenu, ninasema hivi ni kwasababu siku zote huwa siamini kama nitapungukiwa kitu nyinyi mkifanikiwa, na siamini hivyo kwasababu ninajiamini mimi ni mchakarikaji na kipande changu cha KEKI bado kipo mezani kinaningojea ( cha muhimu ni PUMZI na DUA tu ).. ni ukweli tupo kwenye tasnia moja na kila mmoja wetu anajaribu kufanya lile alionalo sahihi ili kusogea mbele, na iko wazi mmeshafanya na mnaendelea kufanya mengi makubwa, nami bila kusita siku zote nimekua ni mtu wa kuwapongeza iwe kwa njia ya mitandao au tukutanapo ana kwa ana.. mie hufanya vile kiroho safi pasina chembe yoyote ya unafiki. ••••••••••••
Nimeyasema hayo hapo juu ili tu uweze au muweze kupata picha halisi ya kilichomo moyoni mwangu na pia kuwakumbusha ya kwamba mimi pia ninao uhuru wa kufanya shughuli zangu za sanaa na yeyote ambaye nimeridhia nae kimaslahi pasina kujali kama jicho la pembeni yangu linaiona faida iliyopo au laah.. sioni ni busara kwa nyie kuja na kujaribu kunipangia yupi nifanye nae au yupi nisifanye nae ili kuwaridhisha machoni/ mioyoni mwenu.. na kama mnaamini ni haki yenu ya msingi mimi kuyafuata hayo matakwa yenu basi naomba nikujuzeni ndugu zangu mtakua mmeonyesha UBINAFSI wa hali ya juu kwenye hili.. pia kumbukeni mimi pia nishawahi kuwa na matatizo na MJENGO.. lakini nilijikuta ninapambana peke yangu hadi UTULIVU uliporejea pasina msaada wa mtu yeyote.. na sikupambana peke yangu kwasababu hamkua na taarifa, taarifa mlikua nazo lakini ninafikiri mlikua mmetingwa na shughuli zenu za ujenzi wa taifa kiasi kwamba hamkuona kama kuniongezea nguvu ingesaidia lile zoezi kuisha haraka.. amini msiamini sijawahi kumuwekea mtu yeyote kinyongo kwenye hilo, na hiyo kitu ilinifunza sana juu ya suala zima la KUJIPAMBANIA MIE MWENYEWE kwenye situation yoyote ile na KUTOKUPIGANA VITA NISIYOIJUA au ISIYONIHUSU.

@babutale PART 2: Yote na yote.. Kiukweli yale maneno ya kwenye promo ya “MOJA KUBWA” sikutegemea kama yangekua na uzito huu uliopelekea ndugu yangu uchafukwe kiasi cha kunifungulia bomba la matusi humu insta.. kwanza sikumbuki hata kama niliyatamka kwa nia ya kuleta msigishano huu.. Lakini kama kweli nimewakwaza... Naomba mnisamehe kibinadamu kwa hilo ,naomba tumuache SHETANI apite na mwisho naomba nimalize kwa kusema.. BURUDANI sio VITA <hivyo ninawatakia kila la heri/ MAFANIKIO ya hali ya juu ktk MAPINDUZI YA BURUDANI huko MTWARA.. KEKI YA TAIFA NI KUBWA SANA NA INA VIPANDE VINGI VINAVYOTOSHA KUMFIKIA KILA ANAYESTAHIKI KWA KUDRA ZAKE MUWEZA WA VYOTE.... MAULID NJEMA 🙏🏾

Jamani Fid Q asamehewe

Mis-leading header..

and am not suprised because wewe ni mmoja kati ya un-educated people wanaoendeshwa na agendas

kwenye hiyo statement ya Fiq-q ni wapi amesema "alikuwa hajielewi" na wapi amesema "hawezi kwenda kinyume na Clouds?"

Yes, ameomba msamaha as a gentleman and he showed his realness side by doing so, but haihitaji akili kubwa sana kuelewa kuwa the entire statement inaonesha kuwa ameamua kuchagua sehemu ambayo inampa faida zaidi.

its a dog eat dog world, and you have to choose the side that benefit you the most in the long run, and yupo kwenye hii industry since 2000's so am sure he knows more and better than your clueless mind ni side gani ambayo inampa au itampa faida kwa muda mrefu.

and bad enough, umeignore statement anayosema he once had problems na Clouds pia but not a single artist supported him.
 
Fid ni mnafiki sana ukimuona kma ana hekima lkn ni snitch mzoefu kuna maneno flan aliyaongea enzi za kampeni nikamshusha kabisa, ingawa Tale nae kazidi uswahili kwan kua na gari ndio kufanikiwa maisha?
 
kwa nini Tale anapenda bifu na CMG..au anamtegemea matako manene..ataumia
 
Mara kwanza sikuamini kama Fid q kaongea hivi as long mwenyewe kakubali ni kweli alikosea kuwaita mafala ,japokuwa aliweka kimafumbo .Tatizo kubwa la wasanii wa Tanzania hawajiamini SUGU kipindi kile ana fight alionekana kama mtukutu na wasanii wakamtenga,Jide nae kajikakamumua mpaka wasanii wenzake wakamtenga lakini akafanikiwa kufanya mambo yake.

Mondi na WCB nao naona wameamua kujitegemea naona wasanii wenzao nao wanampiga vita.Siku zote hauwezi kuwa ww peke yako,ili uwe bora lazima upewe changamoto.Miaka ya nyuma kulikuwa na watu wanaanda matamasha makubwa kaletwa kanda bongoman,brenda fasie,vyone chakachaka,koffi olomide nk na yakafanyika matamasha makubwa.

Ila walivyokuja hawa CMG wakagundua ,kuna baadhi ya mikoa inakosa burudani na ndio maana wakaja na Fiesta na CMG .Kumbuka hata huko nyuma Radio kubwa zilikuwa Radio One na Radio free wakaja wao wakafanya mapinduzi,Hivyo hivyo nao WCB nao wameona fursa wanatakiwa waitumie na kweli wameitumia ,sioni kosa apo japo kuna watu eti wanasema hawana adabu.

Lakini ukitaka kujua fitina za CMG muulize Majizo(wengine Sugu,Jide),hamna mtu aliyekuwa kapigwa fitina tena fitina za kutatisha tamaa kama Majizo,bahati nzuri jamaa mpambanaji mpaka leo hii nae anatamasha lake la KOMAA CONCERT .Wasanii wanatakiwa kuwa kama service provider kwa haya matamasha na kuhusu ubora wa matamasha waachie waandaaji na si kuwa mashabiki kwani kwao haitawajenga kiuchumi,hivi vijembe vya mafumbo havitawasaidia wawachie waandaaji wao ndo wapigane vijembe.
Kweli fid q alizingua kuwatukana
 
Aliongea nini wakati wa kampeni mkuu?
Fid ni mnafiki sana ukimuona kma ana hekima lkn ni snitch mzoefu kuna maneno flan aliyaongea enzi za kampeni nikamshusha kabisa, ingawa Tale nae kazidi uswahili kwan kua na gari ndio kufanikiwa maisha?
 
Fid ni mnafiki sana ukimuona kma ana hekima lkn ni snitch mzoefu kuna maneno flan aliyaongea enzi za kampeni nikamshusha kabisa, ingawa Tale nae kazidi uswahili kwan kua na gari ndio kufanikiwa maisha?
maneno hayo ya kampeni hata mie nayakumbuka,hata mie alinishangaza,hapo kabla nlikuwa namchukulia kama mwana harakati na mwanahiphop anayejielewa kumbe wapii,njaa tu.Bora hata weusi walionyesha msimamo kipindi kile.
 
Back
Top Bottom