Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Leo Agosti 13 ni kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rapa maarufu
Fareed Kubanda, anayejulikana kama Fid Q akiwa amefanikiwa kutoa albamu kadhaa ikiwemo
Propaganda, Roho, Kitaaolojia, na
Mbinguni.
Machi 16, 2020, akizungumza kupitia kipindi cha
Salama Na Fid, kilichokuwa kikiwaendeshwa na Salama Jabir, Fid Q aliwakumbusha watu umuhimu wa kuelewa kampeni na maelezo ambayo wanayapokea kutoka kwa wanaotarajiwa kuwa viongozi wao, akisema;
"Nafikiri ni muda sasa umefika wa watu kuwa wanasikiliza vizuri hizi kampeni zinavyofanywa na maelezo ambayo yanatoka ili waweze kujua wanajihusisha na kitu gani."