Fid Q, Nilistahili Kushinda Tuzo ya Kill

Fid Q, Nilistahili Kushinda Tuzo ya Kill

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

Msanii Fid Q amehabarisha kuwa kila mtu amefurahi kwa yeye kushinda Tuzo ya Mwana Hip Hop Bora wa mwaka , amesema hiyo inajidhihirishahatakwenye Social Media kila mtu anasifia na kukubali ushindi wake. Amasema amebaniwa miaka mingi hiyo tuzo na hatimae ameipata.

Swali:

  • [*=left]Je huko Nyuma ni Kweli watu walikuwa wanabaniwa Tuzo ?
    [*=left]Je Utaratibu Mpya wa Kill Awards kupata washindi ni wa Uwazi zaidi ?
 
Ndio maana Jide anakwambia tuzo halisi za miziki kwa Tanzania bado hazijaanza..
 
Nakua wa kwanza kucomplain kwanini yeye na sio Jo Makini
 
Aanzishe yeye basi hizi zi zilianzishwa na mwwnamuziki mwenzie Dandu R. I. P naye aje na tuzo halisi asiishie tu kuongea.

qn of sheba, mimi ni mshabiki wa jide tena sana lakini nimegundua jide ana tatizo kubwa ngoja niendelee kufanya utafiti nitamtumia salamu hivi karibuni na dawa ya tatizo tunayo sisi mashabiki wake. Ameanza kunikera na nina anza kujuta kumpigia kura.
 
Last edited by a moderator:

Hata mimi pia huwa napenda sana nyimbo zake na twitter huwa nachat nae ila sasa hawa ndugu ukiwaambia ukweli watakuona we ni mamluki umetumwa na clouds ila ukweli kuna some point anakosea... Ni mlalamishi mno muda wote anaona anaonewa yeye at the same point anajiona yeye ni mrs Right hapo tu ndo anaponikera.
 
Last edited by a moderator:
Sababu John Makini haimbi hip hop na ni dhambi kumfanya kuwa msanii bora wa hip-hop,tunzo imekwenda pahala husika

Unaweza kuwa mtazamo, ila sio wa wapigakura Joh ameshawahi chukua hiyo tuzo mwaka 2010 kama sikosei.
 
Napenda sana hip hop, ila nyimbo za FidQ mara nyingi sizielawagi.
 
Hata mimi pia huwa napenda sana nyimbo zake na twitter huwa nachat nae ila sasa hawa ndugu ukiwaambia ukweli watakuona we ni mamluki umetumwa na clouds ila ukweli kuna some point anakosea... Ni mlalamishi mno muda wote anaona anaonewa yeye at the same point anajiona yeye ni mrs Right hapo tu ndo anaponikera.
Ukweli lazima usemwe amezidi deko.
 
Sababu John Makini haimbi hip hop na ni dhambi kumfanya kuwa msanii bora wa hip-hop,tunzo imekwenda pahala husika

Hujui kitu mkuu, hujui hip hop. U much know ndiyo umekukaa kwenye akili yako. Fid q kapewa tu kwa sababu walimbania miaka ya nyuma. Lakini uhalisia fid q hakustahili hata category.
 
Napenda sana hip hop, ila nyimbo za FidQ mara nyingi sizielawagi.

Mmh ila Ney anaeleweka mweh sasa kama nyimbo za fid q hazieleweki za pina zinaeleweka bado utasema ney naye anaimba hiphop na shoga ake kimbunga.
 
Mmh ila Ney anaeleweka mwehsasa kama nyimbo za fid q hazieleweki za pina zinaelewekabado utasema ney naye anaimba hiphop na shoga ake kimbunga.
Mkuu sijakuelewa naomba unifafanulia kwa hatua, hapo naona kama umechanganya hivi.!!!
 
Mkuu sijakuelewa naomba unifafanulia kwa hatua, hapo naona kama umechanganya hivi.!!!

Kama unaijua na kupenda hiphop na hauelewi nyimbo za fid q basi utakuwa unaelewa nyimbo za Ney na Kimbunga.
 
Mkuu nimekukubali unaijua hip hop,Joh Makini haimbi hip hop ana rap tu.

namashaka kama mnaelewa maana ya hiphop. HipHop ni utamaduni au ni jumba ambalo limebebwa na nguzo bila hizo nguzo linaanguka. mfano wa nguzo hizo ni freestyle, graphics, Rap, breakdance na nyingine nyingi , KRS ONE KAZITAJA NYINGI TU. acha tano zinazofahamika.

sasa unaposema Joh hafanyi Hiphop anafanya Rap, unakosea, kwasababu Rap( kugani) imo ndani ya HipHop ni moja ya nguzo ya HipHop tofauti ni kwamba Joh makini anafanya soft Rap( Rap laini) kama wanazofanya wakina Puffdaddy, lily wayne n.k

Fid Q, anafanya hardcore HipHop kama wanazofanya wakina Nas, Talib kweli, Canibus, Immotal Techniques n.k

Mcee. huyu ayejiita the Mcee ndio anabeba maana halisi ya HipHop, kwanza nyimbo zake lazima ziwe za ujumbe na sio mashauzi wala maringo, wala kujigamba gamba hovyo. lakini pia lazima rap style yake iwe kidogo more insisting. lazima ukaze maneno na msisitizo ili ujumbe ufike kwa uhakika zaidi. sisemi usipokaza maneno ujumbe haufiki, lah lakini hautafika kwa msisitizo tofauti na ungekaza maneno.

mtizamo tu.
 
Nakua wa kwanza kucomplain kwanini yeye na sio Jo Makini

Naomba unipe somo kidogo. FidQ kawa msanii bora hiphop wa mwaka 2013/2014 kwa wimbo wake wa "i am a professional", au sio.. Lakini huu wimbo mbona sio wa huu mwaka, infact niwa kitambo kidogo?
Au mimi ndo sielewi mambo haya? Cc Money Stunna
 
Last edited by a moderator:
Naomba unipe somo kidogo. FidQ kawa msanii bora hiphop wa mwaka 2013/2014 kwa wimbo wake wa "i am a professional", au sio.. Lakini huu wimbo mbona sio wa huu mwaka, infact niwa kitambo kidogo?
Au mimi ndo sielewi mambo haya? Cc Money Stunna

wamefanya kumpa tu kutoa lawama,maana umri wake unaenda alistahili hii tuzo kitambo si sasa
 
Back
Top Bottom