Kupiga freestyle kali haikufanyi kuwa mc mkali mbele ya ma'mc ambao hawapingi freestyle, hip hop ni zaidi ya freestyle!!
Ngwair alikuwa mkali Tena Sana ila naona anakuwa overhyped Sana! Alikuwa na flow kali, alikuwa na uwezo wa Kuimba juu ya beat na kuitembelea kama hataki kama Ngoma she got gwan, pia alikuwa ana content Kali zinazoigusa jamii kama a.k.a Mimi au kama ni binti sikiliza ft Jaydee! So ana maunyama yake yaani sio kinyonge! Pamoja na hayo still kulikuwa MC's kibao ambao kiuwezo walikuwa juu ya Ngwair katika namna mbali mbali!!
Mfano huwezi kumuweka Ngwair na Fid kwenye stage Moja halafu ukasema Ngwair mkali kuliko Fid! Tuzungumzie uandishi, matumizi ya lugha, tamadhali za semi, ufundi katika relate na jamii, content zilizoshiba! Watu wanasema Fid anacopy kwenye vitabu, yes hiyo pia ni sehemu pia ya Sanaa na ndio maana MC's wengine hawawezi hiyo! Fid ni knowledgeable! Maarifa mengi! So kete yangu inaenda kwa Fareed Kubanda!