Fid Q Vs Ngwair

Mkuu inaonekana unachanganya rapper mkali na mwanamalenga mzuri. Fid ni rapper anaetegemea zaidi ushairi wa kimapoke pia anatohoa sana hafanyi creation from the scratch. Ila ukija kwenye flow, content, one two one two, ideas bado amuwezi Ngwea. Ngwea anaweza fanya hardcore na commercial ukafurahi. Ila Fid ni underground rap mwanzo mwisho.
 
Fid hawezi storytelling? Report za mtaani ft Zahir Ally Zorro ilikuwa nini? Kwa upande wangu Ile Ngoma ni miongoni mwa Ngoma kali za muda wote as far as storytelling is concerned!
Yeah hawezi ndio maana anayo moja tu. MC bila storytelling hujawa MC mkali.
 
Fareed vingi anavyovirap ni quotes na punch zingine anazifanyia ubunifu kidogo wa kupunguza na kuongezea kama ulisha msikiliza sana Nas na Common utashangaa wanaosema Fid ni mkali zaidi kwa sababu utasikia Nas alishasema kwa lugha ya malikia au Common halafu ena unakuja kumsikia Fid amepita nayo utabaki kujiuliza nani kaitoa wapi?

Hivyo nahitimisha kusema Fareed ni juhudi katika anachokifanya ila Albert ni kipaji
 
Uzito wa mashairi unamaanisha misamiati, misemo na quotes za kwenye vitabu?
Unaweza nitajia wimbo wa Fid Q wenye mashairi mazito kushinda walau jina langu ya Prof Jay?

Wasambaa wanasema “hard work beat talent”

Ngwea anakipaji cha kuweza kutunga wimbo kwa freestyle lakini mashairi yake yatakua mepesi ila yatabebwa na swaga na beat kali anazotumia Ngwea

Fid Q ni aina ya waandishi wanatumia effort kubwa kutunga mashairi na mpangilio
Uandishi huu unahitaji knowledge, ndio maana mnasema ana quote vitabu

Fid Q ana mistari ukiusikia wewe mwenyewe unahisi hajatunga yeye ka copy mahali
Lakink Ngwea anaimba vitu vyepesi kueleweka

Kwa mbele Ngwea ni kama Lil Wyne
Na Fid Q ni kama NAS
 
Kutokujua freestyle Wala sio udhaifu
Fareed,Langa, MwanaFa hata Prof Jay sio wazuri kwenye freestyle.
Wasanii wachache wanaweza kufreestyle na kubandika bars za kueleweka,Ngwair na Afande sele wamo kwenye Hilo kundi.
 
Wiki iliyopita nimesikiliza ngoma za wasanii wote wawili hapo juu
Ngwair nimesikiliza nyimbo 20 na Fareed 25( tokea album Ile ya kwanzA) Zote hizi zipo boomplay.
Mimi naenjoy kuwasikiliza wote na Wala siwashindanishi.
Kila mtu ana ubora wake!!
Ni Kama Hadi Leo naenjoy kuangalia clip za Ronaldinho na Zidane ,wote hao kwangu Mimi ndo Bora kuliko wote na sijawahi hata kufikilia kushindanisha nani mkali
 
Tatizo wabongo wengi wanajifanya wanajua Sana lakini hakuna wanachojua zaidi ya porojo za vijiweni.
Bahati nzuri Fid na Ngwair wote nimewasikiliza since day one wanaanza kutoa Ngoma na kutambulika kwenye game lakini niseme tu hata kumlinganisha Ngwair na Fid NI dhambi kubwa Sana tena Sana.

Binafsi mi ni shabiki mkubwa wa Ngwair Hadi kuna member mmoja hapa JF alizani mi Nina undugu na Ngwair maana hua napenda sana kuchangia Sana nyuzi zinazomhusu Hadi kuandika pia lyrics maana sizani kama kuna Ngoma ya Ngwair sikukalili... Hadi huyo jamaa kwenye simu yake nazani kanisave Ngwair, maana ikifika mahali tukawa marafiki.

Lakini tukirudi kwenye kulinganisha sijajua labda alimaanisha Ngoma zilizobamba club labda kwenye hiyo angle Ila Kama ni swala la Hip-hop basi hapa bongo hakuna msanii anayeweza kumzidi Fid Q labda kidogo kitambo kile Langa Alikua na uandishi mkali tatizo hakua na Ngoma nyingi (consistency) kama Farid.

Kusema anakopi kwenye vitabu huu ni utani Fid anamisemo mingi Sana hata akiwa anazungumza unaweza elewa ni mtu wa namna gani?
"Akikupiga ngumi ya jicho na we mpige ngumi ya sikio akiuuliza unaonaje na we muulize unajisikiaje!?" Sijui huu mstari upo kwenye kitabu gani??
 

Moja ya nyimbo zangu bora za hip hop za mapenzi ni Usinikubali haraka haraka ft Matonya

Kuna mistari flani so amazing
“Sijajipachika kama sticker nimejikita kama tatoo”
 
Umefunga mjadala
 
Ila prof j wengi wataanza kumzungumzia pindi akiwa kasha kuwa marehemu kwasasa design kama wanampotezea hivi. Ila ukizungumzia msaani mwenye uwandishi wa ajabu ambaye hatoki nje ya mada katika kile anachokiimba hakika ni prof j.

Huyu jamaa hakika kujiita prof katika industry ya muziki wa bongo hakukosea, kweli tuwaongelee wakina farid na gwea lakini hawa baba yao ni prof j . Hebu kaa sikiliza hivi vinu vya huyu mwamba
  • usinetenge ft q chifu
  • siyo & ndyo mzee
  • joseph
  • nang'tuka

Afu uje unipinge nikisemacho
 
Professor jay ndo alinifanya nikaipenda hip-hop "chemsha bongo"
Ila Fid Q ndo alinifanya niifatilie hip-hop "Mwanza mwanza"

Professor ni Noma kwenye kuielezea mada moja kwenye wimbo hilo hana mpinzani...
Sauti ya ghetto
Nikusaidiaje
Chemsha bongo

Kuhusu kulinganishwa jamaa alishakataa [emoji2]
 
Nakubal fid q ndo mfalme wa hiphop
 
Namkubali Farid ila Ngwea ni mkali kuliko Farid. Unapozungumzia IQ Ngwea yupo mbele ya Fid Q. Ukimsikiliza Ngwea ngoma zake anaandika flows yani bar after bar zinatililika. Fid hawezi kufanya hata storytelling.
Hatutaki story telling huwa nasikiliza ngoma za Jay z Hana kitu inaitwa story telling ...Ila ni namna mtu anaghani na mashairi fid q is the best
 
Kutokujua freestyle Wala sio udhaifu
Fareed,Langa, MwanaFa hata Prof Jay sio wazuri kwenye freestyle.
Wasanii wachache wanaweza kufreestyle na kubandika bars za kueleweka,Ngwair na Afande sele wamo kwenye Hilo kundi.
Afande sele aliwahi fanya wapi freestyle
 
Kinachokuchanganya ww ni kuchanganyikiwa na mitazamo ya watu wakati ww una mitazamo yako sahihi kabisa alafu kwa kutojiamini unabaki kuuliza ilikuaje.
Ww amini chako ukipendacho mziki ni hisia na tunatofautiana kwenye kusikiliza kile kizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…