Fid Q: Wasanii wananunua views YouTube na wana followers fake mitandaoni

Tafuta maana hata nkikutajia hutazijua mkuu ukipata rudi uniambie kama umezipata tutaanza kumjadili fid q

huwezi,

juzi kaanza kubadilika kaimba roho na bella, ana viewers laki tano.....ushaelewa , bela kambeba

wimbo wake na keisha ( Nalia) na viewers 75k

ni kama wale wanafunzi bora darasani unajua jamaa yule bright sana, nyanga zinapanda ila anaishia kupata C

kwa taarifa yako mimi ni mzee, 94 ni mwanangu wa kwanza! ila nahusika kwa namna moja kwenye biashara ya muziki

ebu nipe song zake kali

FID Q ni kama barnaba wana miss ku connect na watu ili wapae

ha ha ha
 
Fid Q anatafuta kiki kupitia Diamond
 
Fid q anastress huyu..baada kuona madogo wamekuja juzi wanamake money. Ni kawaida ya watanzania tunamchukia MTU aliyefanikiwa
 
Hivi kuna Hit song ipi ya FID Q ambayo kila mtu anaujua?

nyimbo za akina ngwea, prof jay, TMK, Mr. blue, etc zinajulikana hata kama za miaka hiyo

ipi ya FID Q

maana wapenzi wa hiphop wanasema mkali sana, ana mashari balaa, yuko vizuri ..binafsi siyaoni wala sivutiwi na muziki wake na kwa kuuliza hivi ni kutaka kujua

mtu anipe link nifurahie muziki wa FID Q

Ninachoona ni wale die hard wa hiphop ambao wanasema wanabaki kwenye kacha ya hiphop na siyo soko linataka nini
Du mkuu unamzungumzia Fid Q yupi asiekuwa na Hit Song?!

Labda uniambie wewe sio mpenzi wa aina ya muziki anaofanya nitakuelewa.

Pengine kwa msaada Fid Q ni mmoja kati ya wasanii wachache wa Hip hop ambao hawajatoka kwenye misingi waliyoanza nayo lakini Ana mashabiki wa aina zote kuanzia wagumu mpaka wasiopenda hip hop.

Ngoma iliyomtoa huyu na yule imetoka karibu miaka 12 iliyopita kama angekuwa mbovu kama unavyodai unadhani mpaka Leo angekuwepo kwenye chart ya wasanii bora wa Hip hop?!
 
Labda kwa msaada Fid Q ni mmoja kati ya wasanii wachache wa Hip hop ambao hawajatoka kwenye misingi waliyoanza nayo lakini Ana mashabiki wa aina zote.

hit song

ipi????

ipi????

ipi???
 
Tafuta maana hata nkikutajia hutazijua mkuu ukipata rudi uniambie kama umezipata tutaanza kumjadili fid q

huwezi!

ingekuwa Juma nature, haraa haraka ungekumbuka ugali uliokula mchana!

huwezi weka, ni just notion...mkali mkali..mkali

weka wimbo, unaleta blah blah...huwezi, I bet
 
Umofia Kwenu wana JF,

Hiyo ni statement aliyoitoa msanii Fidq wakati akigongesha taya na Dulla Plannet wa E.A Radio wakati akijibu swali kwanini Video zao za wana HipHop hazina View Nyingi na Hawana Followers wengi Insta na Facebook?

FidQ alisema utakuta msanii ana followers zaidi ya milioni 2 lakin iakifanya show hata sebuleni watu hawajai lakini Dr. Jose chameleone ana follower wachache tu ambao kama laki 3 lakini akija tanzania anaweza kupata sponsors wa kutosha na akajaza uwanja wa taifa.

Pili akasema wasanii wengi wananunua view na pia wana followers ambao hawa exist,wanafanya hivyo kwa ajili ya kupata matangazo ya sabuni tu maana makampuni wanaangalia idadi ya followers.

Nakubaliana pia na wazo la fidq wengi wa followers ni ghost utakuta mtu kama lemutuz ana followers kibao lakini akitoa post hapati hata comment kumi.

Anazeeka vibaya,akabidhi kijiti tu kwa wengine.
 
Fid Q anataka kusema kua Akuna Watanzania 7M wanaomiliki smart phone?
Mziki anaoufanya unasikilizwa zaidi na Wagumu, masela wa mtaa ambao hawana habari na Smartphone.
Mtu alale njaa afu ana simu ya 70 Elfu, WAP na WAP?
Darasa wimbo mmoja umemwongezea Followers 2K.
 
Du mkuu unamzungumzia Fid Q yupi asiekuwa na Hit Song?!

Labda uniambie wewe sio mpenzi wa aina ya muziki anaofanya nitakuelewa.

Pengine kwa msaada Fid Q ni mmoja kati ya wasanii wachache wa Hip hop ambao hawajatoka kwenye misingi waliyoanza nayo lakini Ana mashabiki wa aina zote kuanzia wagumu mpaka wasiopenda hip hop.

Ngoma iliyomtoa huyu na yule imetoka karibu miaka 12 iliyopita kama angekuwa mbovu kama unavyodai unadhani mpaka Leo angekuwepo kwenye chart ya wasanii bora wa Hip hop?!

ona sasa sijasema mbovu!!! duh stay kwenye hoja

huyu na yule?? ina tofauti gani na nyimbo kibao za akina mwana FA, AY, king crazy GK, au hawa akina sugu??? nyimbo kama hii ni so common, kimya kimya moja wapo

tena unasema miaka 12 iliyopita na recently huna cha kusema?

'hawajatoka kwenye misingi' ndio hapo mnapomuua....msingi upi usio mpa hela?? fid q hawezi kuja kutamba na kusema anaishi 100% kwa muziki! ney

imagine hizo akili zake, angekuwa anatunga aina ya nyimbo za kama akina 'chemical, darasa, nature, gozdilla, joe makini, niki wa pili, mwana FA...hata akina msodoki...n.k

Tanzanian hip hop usisahau kuna african beat ndani yake ambayo ina miss kwa FID Q, ina maneno machache mepesi ambayo rahisi kueleweka na kuimbika kwa wengine kwa mfano wimbo wa darasa -muziki, nyimbo za akina mr. sugu, prof jay

He need to change na ku focus market , I bet akiamua anawafunika wote hawa maana mashairi yake magumu, mazuri anabaki nayo yeye, au nyie mnaomuelewa ambao hamchangii pato lake kwa namna yoyote ile, hamuendi show zake, hamnunui kazi zake, wala hata tune caller hamjaweka za kwake...bisheni

Joe makini juzi anaungana na chidima, FID Q basi ngau angewaza kuimba na akina rick ross, akon n.k ambako labda anaeleweka vyema, ila kwetu Tandale hata aseme anaweka show bure hakuna wa kuingia, hata akisema anawapandisha watu magari waende hawaendi ng'o....ila kwenu anabaki ndio 'mkali' huyo. Fid q mfananishe na lord eyes ambao uwezo wa na talent zao hawaja link na jamii husika, ila furaha yao ni kuwambiwa nyie ndie wana hipo hop wa 'ukweli'... haya dogo chemical mtoto wa kike amekuja kivingine, waulize jamii wanamkubali nani? mtoto wa kike ana mdondosha huyo mkongwe!

Wimbo gani wa FID Q utauzima ' mtazamo' wa afande sele, prof jay na solo thang, au darubini kali wa afande sele, au hata bwana misosi, au suma G na na vituko uswahilini, au asali wa moyo wa inspecta, sijazisema za juma nature zooote, au niko bize wa jaffarai, au zali la mentali?? wimbo gani wa Fid Q unazika 'hii leo' ya king crazy GK na AY, au Zigo?? ataizika mapozi ya mr. Blue? au nyimbo yoyote ile ya Ngwair ( RIP), Soggy doggy kibanda cha simu?? 'jana na leo' ya stamina na msodoki ...unaifahamu la kuchumpa la kuparama ya Godzilla..au nyimbo zote za Ney wa mitego?..unaijua vituko uswahilini ya suma G? ..Wimbo upi wa Fid Q unauzidi wimbo wowote ule wa darasa?? ...nyimbo zote za darasa zinaimbika mahali popote n watu wote wale..angalia show zake,...zote hizi ziko so close na society zinaimbika..na jamii ndio inayotoa hela, ndio inayolipa...kwa nini habadiliki?

Sio kuwa simpendi maana waswahili hampendi ukweli.......'wazo la leo' stamina ft Fid Q inabaki kuwa best written song kwangu, japo ile chorus ingefanyiwa utundu wa kama ngoma hizo hapo juu tungesema mengine...na utagundua nyimbo za FID alizofanya collabo angalau zina viewers wengi japo si zaidi ya laki sita.....yeye binafsi anabaki na ule ugumu wake 'kuw hawezi saliti hip hop' ha ha ha

ni mtazamo tu
 
Hao followers real unawatambuaje? nadhani ukiwa na followers milioni moja kuna uwezekano mkubwa ukawa na real followers laki tatu..sasa je ukiwa na followers laki mbili real followers ni wangapi?

Hata watoa matangazo wanajiuliza, na sio wajinga.
Word,na hiyo ndivyo ilivyo
 
Nazidi kutokukuelewa...mwanzo kidogo nilikuelewa sasa hivi hueleweki tena.

Oke ngoja tufanye hivi...hoja yako ni kuwa Nyimbo za Fid Q hazimpi hela kama wakina Joh Makini au hoja yako ni kuwa jamaa anafanya muziki mbovu?!
 
Swala la kuwa na followers wengi na ukipiga show hujazi kiwanja sio sababu yenye mashiko kwa m2 anaefikir. Nnavofaham mm ukiwa na followers wengi haimnaish kila ukifanya show ujaze kiwanja coz hao mashabik n wa dunia nzima na sio wa hapa bongo tu.
Kiukweli, sikutegemea kuskia BULLSHIT kama hii kutoka kwa mkali kama fid Q...jupange bro, u can do bigger than this!
 
Nazidi kutokukuelewa...mwanzo kidogo nilikuelewa sasa hivi hueleweki tena.

Oke ngoja tufanye hivi...hoja yako ni kuwa Nyimbo za Fid Q hazimpi hela kama wakina Joh Makini au hoja yako ni kuwa jamaa anafanya muziki mbovu?!

????
 
Umofia Kwenu wana JF,

Hiyo ni statement aliyoitoa msanii Fidq wakati akigongesha taya na Dulla Plannet wa E.A Radio wakati akijibu swali kwanini Video zao za wana HipHop hazina View Nyingi na Hawana Followers wengi Insta na Facebook?

FidQ alisema utakuta msanii ana followers zaidi ya milioni 2 lakin iakifanya show hata sebuleni watu hawajai lakini Dr. Jose chameleone ana follower wachache tu ambao kama laki 3 lakini akija tanzania anaweza kupata sponsors wa kutosha na akajaza uwanja wa taifa.

Pili akasema wasanii wengi wananunua view na pia wana followers ambao hawa exist,wanafanya hivyo kwa ajili ya kupata matangazo ya sabuni tu maana makampuni wanaangalia idadi ya followers.

Nakubaliana pia na wazo la fidq wengi wa followers ni ghost utakuta mtu kama lemutuz ana followers kibao lakini akitoa post hapati hata comment kumi.

huwa naita maneno ya mkosaji kwani hizo deal za matangazo Fid Q hazitaki,wabongo wanafiki sana fanya mziki wakugusa watu wengi uone majibu,Darassa saizi ana views kama m2 naushee
 
Amesema yeye ana followers Real,Hana Fake Followers,Makampuni yanaangalia idadi ya folllowers,yeye hana wengi so si rahisi kupata hayo matangazo ya sabuni.

Mzushi tu ,amejuaje kama followers wake NI real na wengine NI fake ,jamaa akil ndogo ,shida ya wana Muzik wetu hawana elimu so hata ujibuji wao wa maswali unashangaza.
Kama NI rahisi na yeye si atengeneza followes fake ,
 
Back
Top Bottom