Fiesta 2019 Mwanza,Mashabiki watapiga kura na kuchagua wasanii wanaowataka kwenda kufanya show.

Nedago

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2018
Posts
908
Reaction score
1,350
I Hope Mu wazima ndugu wadau,

Nilikuwa Sijasikiliza redio hasa kipindi cha Xxl ya Cloud's fm,kwa muda mrefu sana,
Basi leo nikiwa nawasikiliza nimesikia wakiwahimiza mashabiki wa muziki wa huko Mwanza ambako fiesta itaanzia kwenda kupiga kura na kuwachagua wasanii wanaowataka kuwaona,katika jukwaa la tigo fiesta 2019.

Wamevitaja na vituo ambavyo wanaweza kwenda kupigia kura,pia nimesikia jingles za wasanii wakiomba kupigiwa kura ili waweze kuperform kwenye fiesta msimu huu.

Binafsi naona ni jambo jema na ni ubunifu mzuri waliofanya Cloud's fm,kuwashirikisha hadhira lengwa kuchagua wasanii wanaowataka.

Lakini hii move yao pia itakuwa na negative impacts nyingi sana mfano.

1.clouds fm hawatoweza kutimiza machaguo ya mashabiki wao kutokana na bifu na interests za Cloud's fm,maana kuna wasanii ambao Cloud's haitaki kufanya nao kazi mfano wcb wasafi na wengine wengi tu,na ikatokea wasanii hao ndio walio na kura nyingi je Cloud's itawapeleka kwenye show kutii chaguzi za mashabiki?

2.kama Cloud's tayari wameshaandaa pre-shortlist yao ya wasanii wao ambao inatakiwa wapigiwe kura,na kuwaondoa wasiowataka kwa sababu zao,je kutakuwa na maana gani kama shortlist haikidhi chaguzi za mashabiki?

3.Udhalilishaji kwa wasanii wanaoomba kupigiwa kura,mfano nimewasikia barnaba,mr Blue na dogo janja wakiomba kupigiwa kura,je ikitokea pamoja na kupiga sera zao,halafu itokee wakazi wa mwanza hawajawachagua na Cloud's kuwapiga Chini kufuata chaguzi za wasanii,hao wasanii watajisikiaje hasa kwa next fiesta?

4.Je cloud's wanaweza kumudu kuwaleta na kuwalipa wasanii wote watakaochaguliwa hasa wale wakubwa na wa nje na kuwaleta kwenye show?

Kwa mtazamo wangu ni Vema wangeendelea na utaratibu wao wa kawaida wa kuwapeleka wasanii wao wanaowaona wanafaa baada ya kufanya research yao na kuona ni wasanii gani wanakubarika sana hapa tz,kupitia vipindi vyao vya redio na TV,na kupitia washirika wao wa mwanza na kwingineko,

Huu mfumo haujakaa sawa kabisa na Cloud's hawawezi kutimiza machaguo ya mashabiki kwa asilimia hata 50,ni kama mfumo wa Eatv Award's ulivyofeli kwa kutaka wasanii waombe kushiriki.
 
Kama huo mfumo haujakaa sawa, funguo nawewe redio yako ili tuone huo mfumo ambao upo sawa unakuaje
 
Hivi Wasafi Festival inaweza dumu bila CEO wa WCB?
 
Ni vigumu labda atengeneze wasanii imara zaidi,bu remember hii haiusiani na wcb wasafi.
 
Kama huo mfumo haujakaa sawa, funguo nawewe redio yako ili tuone huo mfumo ambao upo sawa unakuaje
Mkuu kama unaona huna la kuchangia acha wenye uwezo wa kuchambua hili watoe maoni au wewe ni DJ sinyorita?
 
Ubunifu ni muhimu

Ila kuna vitu vingine inabidi viwe simple and clear..
 
Wasanii watakoimba fiesta washapitishwa na kina fauzia...kinachofanyika kunogesha tu hakuna cha kura wala nin.ndo maana umesikia hao madogo wakiomba kupigiwa kura kama kuvutia wauza sato na sangara.
I Hope Mu wazima ndugu wadau,

Nilikuwa Sijasikiliza redio hasa kipindi cha Xxl ya Cloud's fm,kwa muda mrefu sana,
Basi leo nikiwa nawasikiliza nimesikia wakiwahimiza mashabiki wa muziki wa huko Mwanza ambako fiesta itaanzia kwenda kupiga kura na kuwachagua wasanii wanaowataka kuwaona,katika jukwaa la tigo fiesta 2019.

Wamevitaja na vituo ambavyo wanaweza kwenda kupigia kura,pia nimesikia jingles za wasanii wakiomba kupigiwa kura ili waweze kuperform kwenye fiesta msimu huu.

Binafsi naona ni jambo jema na ni ubunifu mzuri waliofanya Cloud's fm,kuwashirikisha hadhira lengwa kuchagua wasanii wanaowataka.

Lakini hii move yao pia itakuwa na negative impacts nyingi sana mfano.

1.clouds fm hawatoweza kutimiza machaguo ya mashabiki wao kutokana na bifu na interests za Cloud's fm,maana kuna wasanii ambao Cloud's haitaki kufanya nao kazi mfano wcb wasafi na wengine wengi tu,na ikatokea wasanii hao ndio walio na kura nyingi je Cloud's itawapeleka kwenye show kutii chaguzi za mashabiki?

2.kama Cloud's tayari wameshaandaa pre-shortlist yao ya wasanii wao ambao inatakiwa wapigiwe kura,na kuwaondoa wasiowataka kwa sababu zao,je kutakuwa na maana gani kama shortlist haikidhi chaguzi za mashabiki?

3.Udhalilishaji kwa wasanii wanaoomba kupigiwa kura,mfano nimewasikia barnaba,mr Blue na dogo janja wakiomba kupigiwa kura,je ikitokea pamoja na kupiga sera zao,halafu itokee wakazi wa mwanza hawajawachagua na Cloud's kuwapiga Chini kufuata chaguzi za wasanii,hao wasanii watajisikiaje hasa kwa next fiesta?

4.Je cloud's wanaweza kumudu kuwaleta na kuwalipa wasanii wote watakaochaguliwa hasa wale wakubwa na wa nje na kuwaleta kwenye show?

Kwa mtazamo wangu ni Vema wangeendelea na utaratibu wao wa kawaida wa kuwapeleka wasanii wao wanaowaona wanafaa baada ya kufanya research yao na kuona ni wasanii gani wanakubarika sana hapa tz,kupitia vipindi vyao vya redio na TV,na kupitia washirika wao wa mwanza na kwingineko,

Huu mfumo haujakaa sawa kabisa na Cloud's hawawezi kutimiza machaguo ya mashabiki kwa asilimia hata 50,ni kama mfumo wa Eatv Award's ulivyofeli kwa kutaka wasanii waombe kushiriki.
 
Asilimia mia ya kura zitawataka wcb na hapa ndio kizaazaa kinapoanzia
 
Wasanii watakoimba fiesta washapitishwa na kina fauzia...kinachofanyika kunogesha tu hakuna cha kura wala nin.ndo maana umesikia hao madogo wakiomba kupigiwa kura kama kuvutia wauza sato na sangara.
You have a point mkuu,ni changa la macho tu.
 
Back
Top Bottom