mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 7,922
- 3,618
Fiesta inampunguzia kasi magufuli kutuletea maendeleo, so ifutwe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jana kulikuwa na ufunguzi wa msimu wa fiesta , na mwamko wa watu ulikuwa mkubwa sana.
Changamoto kubwa ilikuwa kwa waandaaji hasa namna ya uchaguzi wa wasanii waliotumbuiza kuna baadhi ya wasanii hawakustahili kabisa kuwa kwenye jukwaa kubwa kama la jana mfano wasanii kama Nandi, Billnass walionyesha udhaifu mkubwa kulitawala jukwaa labda sababu ya uchanga wao.
Msanii Maua Sama alijitaidi kuimba live lakini bado hakuwa na vibe ya kutosha, aliimba cover nyingi labda kwa sababu ya uchache wa nyimbo zake mwenyewe.
Wasanii wakongwe kama Chege, Madee na Tundaman walijitaidi lakini amsha amsha haikuwa ya kutosha. Kulikuwa na wasanii wengi na tatizo kila msanii alikuwa anaimba nyimbo nyingi hadi inaboa.
Weusi ni moja ya watu wenye shangwe nyingi wanapopanda jukwaani lakini walikuwa na playlist mbovu ya nyimbo zao walishinda kuzipangilia kuleta hamasa.
Msanii mchanga Raymond alifanya vizuri sana alipata shangwe ya kutosha na alijitaidi kwenye connection na mashabiki, Baraka da prince nae alifanya vizuri akiwa nyimbani.
Alikiba alipanda kama suprise nae alifanya vizuri sana japo aliimba wimbo mmoja.
Waandaaji walishindwa kumanage muda Wizkid alipanda jukwaani saa kumi kasaro watu walishakuwa wamechoka ukizingatia walikuwa wamesimama muda mrefu. Wizkid aliimba live na band yake na alilitawala vizuri jukwaa alijiconnect vizuri na mashabiki wake alionyesha kwanini ni msanii star duniani.
NOTE: Wasanii wa Tanzania wanatakiwa kuanza kuimba live band kama tunataka mziki ukue zaidi. Wasanii wa Tanzania wamewekeza zaidi kwenye dancers kuliko kuimba.
Wizkid hakuwa na dancers lakini ile band yake ilijitosheleza kila kitu
View attachment 385166
Ruby kagoma kupiga show akisema Hela ndogomashabiki mnataka show kali wakati wasanii wanaifuata laki kwa basi unazani watapafom show nzuri