Fiesta ndio show inayohudhuriwa na watu very local, mpaka omba omba

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Aisee Fiesta ni show ambayo inakutanisha wasanii wakubwa sana tena wengi kwa pamoja lakini ni show yenye hadhi ndogo kabisa kuwah kutokea. Ni show ambayo mtu mwenyebkipato hutataka kuhudhuria. Ni show ambayo hata mahali inapofanyika hakuna hadhi

Ona list ifuatayo ndio aina ya makundi makubwa yaudhuriao fiesta. Kama unapinga toa facts

1. Boda boda: show ya fiesta ni show inayojaa maboda boda ambao ni watu wa hadhi ya chini

2. Secondary school student: asilimia 50 ya wahudhuriaji wa fiesta ni watoto wa secondary form 1 hadi form 4.

3. Vibaka: siku ya fiesta vibaka wote mjini huudhuria tamasha hilo ambalo wao hutengeneza faida kubwa kwa kuwaibia wengine.

4. Watu walioshindwa shule na kujifanya wanamuziki wakitafuta chimbo la kutoka, fiesta inahudhuriwa na wasanii underground wengi smbao wanatsks kutoka

5. Makahaba wanaojiuza, hawa huwa wote wanahamia fiesta siku ya fiesta ili wapate madanga.

6. Watu wenye hadhi zao ambao huwa ni asilimia moja tu na hii ni kwasababu either wanafanya biashara katika tamasha hili au wamepews kadi za bure za mwaliko na ruge
 
Hao hao ndo wanaowapandisha wasanii. Wenye hadhi zao hawana huo muda.

Hakuna msanii alianza kusikika nje kabla ya kuanza ndani kwanza. Ndio maana hata ukitoka kufanya show kwa wenye hadhi, hupokelewa na kushangiliwa na hao unawaowaita hawana hadhi
 
Uzi umejaa dharau sana huu...

Au hujajua malengo ya fiesta, moja ya malengo ni kuwakutanisha Watanzania wenye rangi tofauti,makabila tofauti,kazi tofauti, hadhi tofauti na kuwafanya wawe kitu kimoja kupitia mziki.
 
Uzi umejaa dharau sana huu...

Au hujajua malengo ya fiesta, moja ya malengo ni kuwakutanisha Watanzania wenye rangi tofauti,makabila tofauti,kazi tofauti, hadhi tofauti na kuwafanya wawe kitu kimoja kupitia mziki.

We ni ruge najua, pole samaki
 
Ifike kipindi tuache majungu.

Bodaboda siyo watu kwani?
Wanafunzi siyo watu?
Vibaka siyo watu?


Kwani hawachangii kiingilio? Wasanii hawalipwi?


Hebu tuondolee utabaka na ubaguzi wa hali za watu, pambana na hali yako. Eti watu wa kipato cha chini, hivi wewe kesho yako unaijua utakuwa na kipato gani hadi uwe na dharau hivyo.

Ya waendaji fiesta waachie wenyewe
 
Ukidharau watuvwa hali ya chini wakati ndio wengi Tanzania na wewe ni mfanyabiashara, Lazima una matatizo! Soko kubwa liko huko. Halafu madharau muache unakuta wanafamilia wako wengi hata bodaboda hawana
 
Ni kweli usemacho kuna siku nilikuwa namfuata dogo m1 alienda fiesta sisi tulikuwa sehemu tukampitia pale leaders njia ya huku kinondoni makaburini. Vibaka walikuwa wengi walichokuwa wakifanya sio ukabaji Bali ni utekaji. Hakuna burudani pale
 
Nikifikiri unasema ipo hivyo kwasababu inahudhuriwa na sisimizi au wadudu.. kumbe binadamu

Wewe utakuwa unawaonea wivu wanaoandaa hiyo show. hauna jingine.. kwa sababu hata hao uliowataja wanalipa kiingilio kwenda kuburudika na ndio dhamira ya Fiesta kuburudiaha haichagui watu.

Kajipige vibao vya usoni ulie wewe masikini wa maishano na rohoni mwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…