FIFA Football Awards 2017: Cristiano Ronaldo achaguliwa kuwa mwanasoka bora wa kiume wa dunia

acha ushabiki mavi kila mfuatiliaji soka anajua kabisa kwa mwaka huu ronaldo anastahili na hana mpinzani kafanya makubwa sana msimu uliopita akiwa na madrid na ureno
Ni sawa mkuu, C. Ronaldo kaiwezesha Ureno kutwaa kombe la ulaya, kaiwezesha RM kutwaa UEFA na kombe la hispania ukiacha na success zingine kibao. Ni ushabiki uchwara tu kusema kwamba hakufanya kitu.
 
Reactions: Pep
Kwa msimu uliopita kiwango chake kilikuwa ni cha kupigania tuzo za EPL peke yake, labda msimu huu Uefa afanye maajabu ili afikiriwe kwa mwakani. Hata medali moja ya club hana! Yaani hata ya kombe la bata!
Ili uwe listed kwenye uchezaji bora ni lazima uwe na mafanikio kwenye ligi na anagalau timu yako ya taifa kwenye michuano mikubwa. Kane hata kuiwezesha spurs kuchukua ubingwa kashindwa, Uingereza kuchukua kombe la ulaya kashindwa sasa tumuweke wapi?
 
Ili uwe listed kwenye uchezaji bora ni lazima uwe na mafanikio kwenye ligi na anagalau timu yako ya taifa kwenye michuano mikubwa. Kane hata kuiwezesha spurs kuchukua ubingwa kashindwa, Uingereza kuchukua kombe la ulaya kashindwa sasa tumuweke wapi?
Labda Mkuu atakuwa amepitiwa, vidole vikateleza kwenye keyboard.
 
Nyota wa Real Madrid ameshinda tuzo hiyo kwa mwakwa wa pili mfululizo baada ya kuwaongoza Blancos kutwaa Liga na Ligi ya Mabingwa



Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bora wa FIFA wa mwaka upande wa wanaume 2016-17.


Ronaldo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kufanikiwa kuwashinda Neymar na Lionel Messi katika sherehe za tuzo hiyo mjini London.


Mreno huyo, 32, alipata mafanikio makubwa katika kampeni za 2016-17 kwani aliwaongoza Blancos kutwaa taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.


Messi, kwa upande wake alifunga magoli 54 katika mechi 52 kwenye michuano yote msimu uliopita, lakini alifanikiwa kutia taji moja tu mikononi mwake, Copa del Rey akiwa na Barca - na ni mataji tu ya Madrid yaliyomwezesha nyota wao kutwaa tuzo hiyo maarufu.


"Asanteni sana, kwa wale wote walionipigia kura. Sina budi pia kuwataja Leo na Neymar kwa kuwa hapa," Ronaldo alisema baada ya kupokea tuzo.


"Real Madrid, Kocha, mashabiki na rais - kwa ushirikiano wenu wote kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru sana.


"Nimefurahi sana kutwaa tuzo hii mfululizo. Huu ni wakati mzuri sana kwangu. Shukrani nyingi sana kwa mashabiki kote duniani kwa kuniunga mkono. Nashukuru sana kwa hilo.


"Inapendeza kuwa hapa na wachezaji hawa wakubwa, na nimefurahia sana, asanteni sana."

Tuzo ya Mchezaji bora wa kiume ya FIFA awali ilikuwa na orodha ya majina ya watu 24 yaliyotangazwa Agosti.


Kutokea hapo Ronaldo, Messi na Neymar walitajwa kuwa majina matatu ya mwisho Septemba.


Mshindi wa tuzo hiyo alichaguliwa na makocha wa sasa kutoka kwenye kila timu ya taifa ya FIFA kwa wanaume, manahodha wa kila timu ya taifa, na waandishi wa habari kutoka kila ukanda unaowakilisha timu ya taifa na mashabiki wote duniani waliojisajili kwenye tovuti ya FIFA.com.


Ronaldo alitwaa pia tuzo ya mchezaji bora wa FIFA 2016. FIFA hapo awali walikuwa wakitoa tuzo ya Ballon d'Or kwa ushirikiano na France Football, lakini pande hizo mbili zilitengana mwaka jana.


France Football bado linatoa Ballon d'Or na inatarajiwa kuwa Ronaldo ataifikia rekodi ya Messi kwa kutwaa tuzo ya tano tuzo hiyo itakapotangazwa Desemba.


Mchezaji bora wa FIFA wa mwaka haikuwa tuzo pekee ya heshima kwa Ronaldo katika usiku wa Jumatatu, lakini pia alitajwa kwenye FIFPro World 11 kwa mwaka wa 11 mfululzo.


Straika wa Arsenal Olivier Giroud alishinda tuzo ya Puskas ya FIFA kwa goli bora la msimu wa 2016-17, Bosi wa Real Madrid Zinedine Zidane akichukua tuzo ya kocha bora wa mwaka, na veterani wa Juventus Gianluigi Buffon akitwaa tuzo ya kipa bora wa FIFA.


Ronaldo amefunga goli moja La Liga katika mechi tano msimu huu wa 2017-18, lakini amefanikiwa kufunga mara tano kwenye michuano ya Ulaya katika mechi tatu tu.

Pia katika tuzo hizo Gianluigi Buffon alishinda golikipa bora wa mwka, Olivier Giroud akishinda goli bora la mwaka na Zinedine Zidane akiwa kocha bora wa mwaka


Chanzo: Goal .com
 
Ronaldo hamna kitu Ila ndio mshindi. Bure kabisa


Acha Usukule! Hizi Tunzo ni Za Msimu Uliopita Ambao Ronaldo Alionesha Mchango Mkubwa Katika Mafanikio Kwa Club Yake na Real Madrid...

Msimu Huu Ni Kweli Hamna Kitu hapo upo sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…