FIFA kuondoa offiside na kubadili upigaji wa penati

Hii ya offside itasababisha beki hata acheze miaka kumi hataweza kufunga labda ajifunge golini kwake, pia swala la kushika ikiwa kadi ya njano kwa mpira uelekeao golini basi kihesabike ni goli
 
Penalty , offside na Substitution zibaki kama zilivyo. zinaleta raha sana na ushindani mchezoni
 
Kitu kingine ninacho ina kinafaa kubadilishwa ni timu zikitoka dare mpaka dakika ya 90 basi katika muda wa nyongeza waingie kwanza wachezaji waliokuwa bench na nafasi zitakazo baki zijazwe na waliotoka itapedeza kushirikisha wote
 
filipo inzaghi,rud van neestoroy, nuno gomes

jamaa warud tu kwenye sheria mpya ikifutwa offside kila mechi watatupia goli mia
 

Nimezipenda hizo 3;

1. Kupunguza adhabu mipira ya kushika
2. Kapteni awe ndo mtu pekee kuongea na refa
3. Sub zifike 5
 
Ya offside wamechemsha coZ striker atakua anashinda na golikipa wanapiga story...wangeruhusu pia waingie na kahawa au chai wawe wanashushia huku striker anasubiri amalizie tu, itapendeza zaidi

Kwani Mabeki nao watalala?, nao si wataweka ulimzi, ni badiriko zuri tu, kwani hata lile la Kipa kutodaka backpass nalo lilikuwa gumzo na ilionekana kuwa litakuwa zoezi gumu, lakini limefanikiwa kwa ustadi mkubwa na wachezaji wameadapt vizuri tu
 
Kuondoa Offside Kutafanya Washambuliaji WAVIVU Kama CHIRWA na KICHUYA Kukaa na Golikipa Kwa dakika zote 90
 
La offside siliafiki,kuongeza sub na kupunguza adhabu kwa mpira wa kushika na kurefusha sehemu ya kupigia penati ni mawazo mazuri.Na hata hiyo ya nahodha kuwa ndio muongeaji na refa ni wazo zuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…