FIFA kuondoa offiside na kubadili upigaji wa penati

Soka Bila Ya Offside?? Sasa ni Wakati Mzuri Wa Kumsajili Usain Bolt....
 
Huyu jamaa atapunguza ladha ya mpira, itafika hatua mwisho wa msimu mchezaji ana magoli 300 na ladha itakua ni ndogo sana. Football iachwe ivo ivo except ilo suala la kupunguza adhabu nalo ni muhimu. Wakati mwengine mchezaji anakua hana alternative way na wakati mwengine mchezaji anafanya kwa bahati mbaya unakuta amepigwa red card
 
Yaani mtu ashike mpira kama ule wa Suarez halafu apewe kadi ya njano? Hapana kwakweli.
Ni kuiongezea machungu tim pinzani.
 
Hapo offside ni kuharibu soka hata kwenye penalt pia.zibaki sheria hizi hizi
 
la offside nalipinga, nahishi wanachezaji pinzani watakuwa nanasubiri mpira golini
Yaani wakiondoa offsides mafoward wanakaa ndani ya kumi 18 hawatoki na mabeki hawapandi.... Mpira utachezwa na viungo tu
 
Wewe siyo mshabiki wa soka, utakuwa mshabiki wa netball ww!
 
cungi mkono hata moja, ye anafanansha basket na football??
 
Yanatakiwa yapitishwe fasta kabla hatujakutana nao, na hivi mwenyekiti wao amevurugwa tutaivunja rekodi yetu tuliyoiweka kwa kandambili
Teh teh teh.
 
Hili ofside huwa naliota kila siku...hii sheria huwa inakuaga na mikanganyiko mingi sana.
 
Mabeki itabidi wale nao sahani moja, wakiwasahau imekula kwao!

Kuondoa Offside Kutafanya Washambuliaji WAVIVU Kama CHIRWA na KICHUYA Kukaa na Golikipa Kwa dakika zote 90
 
This is a joke right? Sidhani kama raisi wa fifa ni mpuuzi kiasi hiki
 
Kitu cha maana hap0 ni kupunguza adhabu ya handba na kuongeza sub.vingine vitaharibu ladha ya mchezo.
Mkuu mi naogopa hapo kwenye offside, kutazalisha magoli mengi na kuharibu kabisa ladha mchezo wenyewe
 
Kuondoa offside hii ina changamoto nyingi sana, kwa kawaida wakati offside inatumika wachezaji walikuwa wanacheza half moja karibu muda wote wa mchezo kuogopa kuotea, sasa kwa zile km 8-12 average coverage za mchezaji kukimbia zitaongezeka mara 2 na hii inaweza kusababisha wachezaji kuzimia au muda mwingi watakuwa wanatembea wakiwa na mpira uwanjani na sio kukimbia kama ilivyo kuwa radha ya kabumbu, hivyo option ni tatu
1.wapunguze muda wa mchezo sema dk 60
2. waongeze idadi ya wachezaji kufika 20 kwa timu moja au
3. wapunguze ukubwa wa uwanja labda iwe upana kwa urefu 40*60

kwa hizo option tatu kwangu itakuwa ni ujinga mkubwa katika ulimwengu wa soka, kwa maoni yangu offside ihesabike angalau mita 3 kutoka kwa beki wa mwisho na sio kama sasa yaani mkono tu ni offside
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…