John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kwa pamoja wametangaza kuzifungia timu zote za Urusi katika michuano ya kimataifa kuanzia ngazi ya klabu hadi timu za taifa hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.
Mamlaka hizo za soka zote zimetoa tamko la pamoja, hiyo inamaanisha kuwa Urusi imeondolewa katika mbizo za kushiriki Kombe la Dunia Qatar 2022.
Maamuzi hayo yanafikiwa kutoka na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuagiza majeshi yake kushambulia Ukraine, hivi karibuni.
Hivyo, Urusi haitashiriki katika mchezo dhidi ya Poland uliopangwa kuchezwa Machi 24, 2022 na timu ya soka ya wanawake itakosa michuano ya Euro 2022.
FIFA na UEFA wamesisitiza kuwa soka ni mchezo wa umoja na amani ambapo pia UEFA imevunja mkataba wa udhamini wa paundi milioni 33.5 wa Kampuni ya Gazprom ya Urusi.
Source: The Sun