Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kikosi bora cha Kombe la Dunia 2026 (FIFA Dream XI), ambacho kimepatikana kupitia kura za mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kikosi hicho kinamjumuisha kipa Vozinha (Cape Verde), mabeki Pedro Porro (Hispania), Lisandro Martínez (Argentina), Dayot Upamecano (Ufaransa) na Marc Cucurella (Hispania).
Safu ya kiungo imeundwa na Rodri (Hispania), Michael Olise (Ufaransa) na Jude Bellingham (England), huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Lionel Messi (Argentina), Erling Haaland (Norway) na Kylian Mbappé (Ufaransa). Kikosi hicho kimetangazwa chini ya kauli mbiu ya "The Fans Have Spoken", ikimaanisha kuwa uchaguzi umefanywa na mashabiki kupitia kura zao.
Mdau, una maoni gani kuhusu kikosi hiki? Kuna mchezaji ambaye unadhani alistahili kuwemo lakini ameachwa?