Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mashabiki wa Joao Pedro tunafurahia sana anguko la Brazil maana si kwa chaguzi za kipuuzi namna ile kwa wachezaji wa WC 2026.Brazil wameshindwa kutoa mchezaji ni anguko kubwa kwaJoao Pedro fans
Laana ya kumuacha Romalio kwenye WC ya mwaka 2002 inaendelea kuwatafuna,Labda wakatubu .Brazil wameshindwa kutoa mchezaji ni anguko kubwa kwao
Romero badala ya Upemecano.
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kikosi bora cha Kombe la Dunia 2026 (FIFA Dream XI), ambacho kimepatikana kupitia kura za mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kikosi hicho kinamjumuisha kipa Vozinha (Cape Verde), mabeki Pedro Porro (Hispania), Lisandro Martínez (Argentina), Dayot Upamecano (Ufaransa) na Marc Cucurella (Hispania).
Safu ya kiungo imeundwa na Rodri (Hispania), Michael Olise (Ufaransa) na Jude Bellingham (England), huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Lionel Messi (Argentina), Erling Haaland (Norway) na Kylian Mbappé (Ufaransa). Kikosi hicho kimetangazwa chini ya kauli mbiu ya "The Fans Have Spoken", ikimaanisha kuwa uchaguzi umefanywa na mashabiki kupitia kura zao.
Mdau, una maoni gani kuhusu kikosi hiki? Kuna mchezaji ambaye unadhani alistahili kuwemo lakini ameachwa?
Laana ipi hiyo mbona walibeba kombe hiyo 2002. Hawa wameacha kucheza pira lao asilia (Samba) wameanza kucheza pira la kigeni(maelekezo).Wenzao Argentina hawaachi kucheza pira lao la kitaa a.k.a Ndondo na wanapeta tuLaana ya kumuacha Romalio kwenye WC ya mwaka 2002 inaendelea kuwatafuna,Labda wakatubu .
Labda wameangalia saves za hatari zaidi. Unai Simon watu walikuwa hawafiki golini kwake mara kwa mara. Imagine Argentina hawakupiga shot on target hata moja. Team work imembeba sana!. Hajakutana na real challenge ya kupima uwezo wake!Kikosi kimekaa kisiasa sana. Mfano mdogo tu, golikipa aliyestahili kuwepo kwenye hicho kikosi ni Unai Simon wa Spain.
Mbona walichukua WC 2002?Laana ya kumuacha Romalio kwenye WC ya mwaka 2002 inaendelea kuwatafuna,Labda wakatubu .
Mkuu,kama ingekua ni laana kumuacha Romario WC2002 basi Brazil wasingechukua kombe la World Cup mwaka huo,Laana ya kumuacha Romalio kwenye WC ya mwaka 2002 inaendelea kuwatafuna,Labda wakatubu .
Weka cha kwako au tuambie nani alistahili kutoka hapo uweke mchezaji wakoKikosi cha hovyo.
Mashabiki wa yule mzee wa Portugal hao.Weka cha kwako au tuambie nani alistahili kutoka hapo uweke mchezaji wako
Unai alikuwa hashambuliwi kutokana na aina ya uchezaji wa SpainKikosi kimekaa kisiasa sana. Mfano mdogo tu, golikipa aliyestahili kuwepo kwenye hicho kikosi ni Unai Simon wa Spain.