- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Madai
Ukurasa rasmi mmoja kutoka mtandao wa Instagram umechapisha ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ukiitaka klabu ya Simba SC na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumpendekeza Clatous Chama kwenye tuzo ya goli bora (Puskas).
Uhalisia
Picha iliyoambatanishwa kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii imetengenezwa kwa njia ya kidijitali (manipulated/edited) na si ya kweli. FIFA hawajawahi kupost ujumbe huo kwenye ukurasa wao wa Instagram au mtandao mwingine wowote.
Zifuatazo ni alama za wazi zinazoonyesha picha hiyo imetengenezwa.
Muundo wa herufi (Font na Alignment): Mpangilio wa herufi na nafasi (spacing) kati ya jina la akaunti na ujumbe haziendani na mfumo rasmi wa Instagram.
Kanuni za Tuzo ya Puskas: FIFA haiombi klabu au mashirikisho ya nchi kupitia "post za Instagram" kupendekeza magoli. Kuna jopo la wataalamu na mfumo rasmi wa kisheria unaokusanya na kuchuja magoli bora duniani kote kwa ajili ya tuzo hiyo.