sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Hii ni baada ya CAS kuiamuru Etoile Du Sahel kuilipa Simba Sc USD 300,000. Kiasi hicho kilikuwa ni kwa ajili ya uhamisho wa Okwi. Simba Sc iliamua kwenda CAS baada ya Etoile du Sahel kugoma kulipa ada ya uhamisho ikidai kua ina hali mbaya kiuchumi.
NB: "zaidi ya usd 300,000 + mkwanja wa mtani jembe + vyanzo vyetu vya mapato = Simba Sc Complex mitaa ya Bunju"
===============
===============
NB: "zaidi ya usd 300,000 + mkwanja wa mtani jembe + vyanzo vyetu vya mapato = Simba Sc Complex mitaa ya Bunju"
===============
===============
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.
Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28.
[TD="align: center"][/TD]
[TD="align: center"]OKWI (KUSHOTO) WAKATI AKIICHEZEA ETOILE KATIKA LIGI YA TUNISIA[/TD]
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.
Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28,000.
Hatua hiyo imefikia baada ya Simba kushinda kesi iliyotokana na Simba kushitaki kwa Fifa baada ya Etoile kushindwa kulipa fedha za malipo ya kumnunua Emmanuel Okwi.
Okwi aliuzwa wakati wa uongozi wa Ismail Aden Rage na Etoile ikautumia mwanya huo kuanza kuizungusha Simba.
Rage aliahidi Etoile wangelipa wakati akiwa madarakani, kabla hajaondoka, lakini haikuwa hivyo.
Zigo likamuangukia yeye kwa kuwa ndiye aliidhinisha Okwi kwenda Etoile hata kabla ya Waarabu hao kulipa, kabla ya kumgeuka.
Etoile walizidi kusumbua baada ya Okwi kurejea Uganda na baadaye Yanga, hali iliyofanya Simba kukata tama.
Taarifa zinaeleza barua ya agizo hilo, tayari imetua TFF ambayo imewasilisha kwa Rais wa Simba, Evans Aveva kwamba anatakiwa kupokea mzigo pamoja na faini hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Tayari Okwi ameisharejea Simba akitokea Yanga, hivyo Simba itafaidika kuwa na mchezaji halafu na mkwanja juu.
SalehJembe BLOG
