FIFA yaiagiza Etoile Sahel kuilipa Simba fedha za usajili wa Okwi

FIFA yaiagiza Etoile Sahel kuilipa Simba fedha za usajili wa Okwi

Subiri utakachoambiwa na kina Aveva na Kasim Dewji. Watakuambia hizo pesa wala hazitoshi kulipa madeni ya klabu. Watakuambia kuwa hata hao wachezaji wanaosajiliwa ni kwa fedha za mkopo kutoka kwa hao wanaojiita wafadhili au friends of simba na sio kutoka klabuni.

Sidhani kama kutakua na execuse ya madeni, maana ktk mechi saba tu za ligi tumeingiza zaidi ya 190m mapato, kuna jengo la klabu ambalo ni chanzo cha mapato, kuna hela za udhamini toka TBL n.k sasa hayo madeni yatatoka wapi?
 
Hiyo pesa haifiki hata TZS 1bn/= wewe unazungumzia kujenga uwanja! Heri kuwa kipofu wa macho kuliko kuwa kipofu wa akili (ujinga).

560m za Etoule + 100m Za MJ + 200m Kodi Za Jengo + 300m Michango Ya Wanachama = 1.16 Bilioni

Mungu bariki hii projekiti isije ikawa kama ile ndoto ya kutaka kujenga uwanja katika Bwawa la Jangwani.
 
Sijui shafih dauda ataongea nini tena maana alishaapa na wenzake wa sports xtra kuwa rage alishapiga mpunga...
 
Sijui shafih dauda ataongea nini tena maana alishaapa na wenzake wa sports xtra kuwa rage alishapiga mpunga...

Dah, kweli umenikumbusha AISEE. Ila hawa jamaa waga hawana AIBU atauchuna TU. Wangekuwa wengine wangeweka ile sehemu waliyomrekodi kwamba alisema UONGO ila kwa kuwa ni wao wenyewe watauchuna TU.
 
UZI HUU ni wa WANA MSIMBAZI CHAMA KUBWA-TAIFA KUBWA,kandambili mnataka nini humu,mbona nyie ule mradi wenu na ridhizani mpaka leo bado pale kisiwani,kila kitu mmpa riz1
 
Dah, kweli umenikumbusha AISEE. Ila hawa jamaa waga hawana AIBU atauchuna TU. Wangekuwa wengine wangeweka ile sehemu waliyomrekodi kwamba alisema UONGO ila kwa kuwa ni wao wenyewe watauchuna TU.

Mpaka sasa nimejaribu kuperuzi katka blog yake kauchuna kimya utadhani hakuna kitu kilichotokea.
 
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.

Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28.

[TD="align: center"] [/TD]

[TD="align: center"]OKWI (KUSHOTO) WAKATI AKIICHEZEA ETOILE KATIKA LIGI YA TUNISIA[/TD]

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.

Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28,000.

Hatua hiyo imefikia baada ya Simba kushinda kesi iliyotokana na Simba kushitaki kwa Fifa baada ya Etoile kushindwa kulipa fedha za malipo ya kumnunua Emmanuel Okwi.

Okwi aliuzwa wakati wa uongozi wa Ismail Aden Rage na Etoile ikautumia mwanya huo kuanza kuizungusha Simba.

Rage aliahidi Etoile wangelipa wakati akiwa madarakani, kabla hajaondoka, lakini haikuwa hivyo.

Zigo likamuangukia yeye kwa kuwa ndiye aliidhinisha Okwi kwenda Etoile hata kabla ya Waarabu hao kulipa, kabla ya kumgeuka.

Etoile walizidi kusumbua baada ya Okwi kurejea Uganda na baadaye Yanga, hali iliyofanya Simba kukata tama.

Taarifa zinaeleza barua ya agizo hilo, tayari imetua TFF ambayo imewasilisha kwa Rais wa Simba, Evans Aveva kwamba anatakiwa kupokea mzigo pamoja na faini hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Tayari Okwi ameisharejea Simba akitokea Yanga, hivyo Simba itafaidika kuwa na mchezaji halafu na mkwanja juu.

SalehJembe BLOG
 
Dah, kweli umenikumbusha AISEE. Ila hawa jamaa waga hawana AIBU atauchuna TU. Wangekuwa wengine wangeweka ile sehemu waliyomrekodi kwamba alisema UONGO ila kwa kuwa ni wao wenyewe watauchuna TU.

wanajifanya wajuaji sana
 
Hii ni baada ya CAS kuiamuru Etoile Du Sahel kuilipa Simba Sc USD 300,000. Kiasi hicho kilikuwa ni kwa ajili ya uhamisho wa Okwi. Simba Sc iliamua kwenda CAS baada ya Etoile du Sahel kugoma kulipa ada ya uhamisho ikidai kua ina hali mbaya kiuchumi.

NB: "zaidi ya usd 300,000 + mkwanja wa mtani jembe + vyanzo vyetu vya mapato = Simba Sc Complex mitaa ya Bunju"

===============
===============

Mkuu sembo naomba update, fedha ya Okwi ilitakiwa iingie lini kwenye akaunti ya Simba? Lini imeingizwa?
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama kutakua na execuse ya madeni, maana ktk mechi saba tu za ligi tumeingiza zaidi ya 190m mapato, kuna jengo la klabu ambalo ni chanzo cha mapato, kuna hela za udhamini toka TBL n.k sasa hayo madeni yatatoka wapi?

Hela tayari mmepata?
 
Bado tunangoja umalize kuoka mikate Azam.Ikiingia utaifeel tu usiwe na haraka.
 
Back
Top Bottom