FIFA Yamfungia Maisha Mwamuzi Kutoka Tanzania, Oden Charles Mbaga

FIFA Yamfungia Maisha Mwamuzi Kutoka Tanzania, Oden Charles Mbaga

Yaani umeishamfungia mtu maisha na mifaini ya mahela yote hayo,hapo n kupiga kimya.

Sent from Nokia 7 Plus
Mimi nisingewajibu kitu pesa yote hiyo labda abet ndio ataipata
 
View attachment 1032917
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imemfungia maisha mwamuzi wa zamani wa kimataifa ambaye pia ni Katibu wa Chama Cha Waamuzi Tanzania (FRAT) Oden Charles Mbaga kwa kujihusisha na masuala ya rushwa ya upangaji matokeo.

Aidha Mbaga anatakiwa kulipa faini ya kiasi cha fedha ya Uswis Faranga 200,000 (Zaidi ya shilingi milioni 468 a Kitanzania) ndani ya siku 30 tangu amepata taarifa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TFF, Uamuzi huo unafuatia uchunguzi uliofanyika kuanzia Julai 11, 2018 ambapo Mbaga amekutwa na hatia ya kuhusika kwenye upangaji wa matokeo ikiwa ni kinyume na kanuni za maadili za FIFA.

“Anafungiwa maisha kutojihusisha na shughuli zozote za mpira wa miguu katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 7j ya Kanuni za Maadili za FIFA za mwaka 2018 pamoja na Ibara ya 22 ya Kanuni ya Nidhamu ya FIFA,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mwamuzi huyo anaweza kukata rufaa kwenye mahakama ya kimichezo ya FIFA (CAS) ndani ya siku 21 tokea maamuzi yalipofanyika na ndani ya siku 10 baada ya kumalizika siku 21.

Source: fifa.com
Adjudicatory chamber of the independent Ethics Committee sanctions Oden Charles Mbaga

Sent using Jamii Forums mobile app
Kalipa huo mzigo?
 
Back
Top Bottom