FIFA yasitisha rasmi kuja Tanzania na imebariki maamuzi ya Kisheria ya Mahakama dhidi ya Malinzi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wallace Karia ambaye kwa sasa ndiyo anakaimu nafasi ya Urais wa TFF amethibitisha kuwa ule Ujumbe maalum wa FIFA uliokuwa uje nchini Tanzania kufuatilia sakata zima la Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi na Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa sasa umesitisha na kusema kuwa hautakuja tena nchini Tanzania na kwamba wanaiachia Mahakama ya Tanzania ifanye Kazi yake.

Source ya habari hii ni Efm Kipindi cha Sports Headquarters ambacho kimeanza hivi punde tu na Kiongozi huyo ataongea kiundani zaidi ndani ya dakika 15 zijazo hivyo ni vyema kama upo karibu na Redio yako basi uka tune in Efm usikilize.

Nimalizie tu kwa kusema pole sana kwa Jamal E. Malinzi na wale Team Malinzi wote. Ngoma inogile.

Nawasilisha.
 
Fifa ya blatter na CAF ya Issa hayatou ndio zilikuwa zinaziba mabaya yao yote kuzuia serikali zisiingilie michezo, hiyo yote ilikuwa njama ya kulinda ubadhirifu wao
 
Sio jambo la ajabu, ni utaratibu, wacha mahakama zifanye kazi zake. Rushwa na ubadhirifu na vitendo vibaya sana vinavyopaswa kukemewa na kila mzalendo.
 
FIFA hawawezi kuingilia kesi za jinai ingalikuwa ni kesi zinahusu mambo ya michezo ingekuwa sawa ila money laundering ni kesi purely ya jinai
 
"......Source ya habari hii ni Efm Kipindi cha Sports Headquarters ambacho kimeanza hivi punde tu na Kiongozi huyo ataongea kiundani zaidi ndani ya dakika 15 zijazo hivyo ni vyema kama upo karibu na Redio yako basi uka tune in Efm usikilize."

Wengine hiyo Efm haishiki mkoani kwetu mkuu kwa hiyo kama unaisikiliza ni vyema ukaendelea kutupa updates
 

Sawa Mkuu ila naamini wana JF wengi ni wapenda mpira / soka hivyo hata wao pia watasaidia kukupa updates humu za hii taarifa na naomba pia ushirikiano wao kwani hata Mimi siyo kila mara nakuwa nasikiliza Redio.

Mambo au Utamu wote juu ya hili upo Efm katika Kipindi kizuri cha Sports Headquarters ambacho kipo ' mubashara ' hivi sasa.
 
poa sana mkuu..pamoja
 
Hivi Jana si uliahidi ungeleta taarifa rasmi SAA tano!
Mbona ulipotea moja kwa moja?
 
Hivi Jana si uliahidi ungeleta taarifa rasmi SAA tano!
Mbona ulipotea moja kwa moja?

Nilisema kuwa ningerudi tena JF muda wa Saa 5 usiku na muda ule nilioleta huu uzi ulikuwa ni Saa 3 kamili na kuna mahala nilikuwa nawahi. Suala siyo kuleta taarifa rasmi bali nilisema nitarudi ili tuendelee ' kuyajenga ' juu ya hili. Na cha ' kuchekesha ' kale ' Kabinti ' Makamu wa Kamati ya Uchaguzi kamesikika kakisema kuwa ' Yeye ' hana hiyo taarifa wakati ' waliovujisha ' hii taarifa ambayo bado inafanywa ' Siri ' ni hao hao ' Wajumbe ' wa Kamati hiyo pamoja na mmoja wa Mawakili wake kati ya wale Watano wanaomtetea Malinzi.

Nadhani TAKUKURU / PCCB iwakamate na hawa ' Wajumbe ' wanne ( 4 ) wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambao wanampigia ' chapuo ' Rais Malinzi ili wawahoji vizuri ' Kinjagu ' kwani yawezekana kuna ' chenji chenji ' ya Pesa anazotuhumiwa nazo Malinzi na wao ' wamegawiwa '.

Tusipoangalia hawa ' Wajumbe ' wabishi wanne ( 4 ) wa Kamati ya Uchaguzi Mkuu wa TFF wanaweza ' wakatucheleweshea ' maendeleo ya mpira wetu Tanzania na sidhani kama wana nia njema na mpira wa Tanzania kwani wamekaa ' Kimahaba ' na ' Kimaslahi ' zaidi.
 
imebariki kipi ikwa haiko na evdence vile haikuja
 
imebariki kipi ikwa haiko na evdence vile haikuja

Kaimu Rais wa TFF Wallace Karia ameshawatumia kila kitu kinachoendelea huko Mahakamani na bado mpaka sasa wanawasiliana nae. Na ndiyo maana nimewaombeni kuwa sikilizeni Efm sasa hivi ili mpate ' ufafanuzi ' mnaoutaka.
 
endeleeni kutujuza yanyozungumzwa kupitia EFM maana wengine tupo mikoa ambayo EFM haikamati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…